HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 11 July 2018

WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI

NA TIGANYA VINCENT
KAMPUNI  na wadau mbalimbali Mkoani Tabora wameomba kusaidia ujenzi wa nyumba kwa ajili ya  Askari Polisi ambao wanakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi na hivyo kulazimika kupanga uraini.

Ombi hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akipokea msaada wa mifuko 600 za Saruji zenye thamani ya milioni 10,800,000/- uliotolewa na Kampuni ya  ununuzi wa Tumbaku ya Alliance One.

Alisema kuwa Askari wengi wa vyeo vya chini wanalazimika kupanga uraini jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linapunguza ufanisi katika kupambana na uhalifu.

Mwanri alisema kwa mujibu taarifa za Askari  Polisi inaonyesha kuwa Polisi wapatao 853 wanaishi uraiani na wanaoishi kambini ni 327 jambo ambalo sio zuri katika kuleta ufanisi wa utendaji wa Jeshi hilo.

Alisema mpaka hivi sasa jitihada za awali za kuandaa michoro ya ramani za nyumba ambazo zinatarajiwa kujengwa na hivyo kuwaomba wafanyabiashara, Kampuni kujitokeza kuchukua kwa ajili kuwajengea kwa kadiri watakavoweza.

“Tuko kwenye kampeni ya kuwajengea vijana wetu Polisi nyumba za kuishi …tunaomba safari hii badala ya kutuletea vifaa kama vile saruji, nondo , bati mtusaidie kujenga nyumba za askari Polisi na mutukabidhi vifunguo mkishamaliza kujenga …asakari wetu wengi hawana nyumba na hivyo kulazimika kuishi uraiani…tunawaomba Alliance One, Kampuni nyingine na  wadau watakaoguswa na tatizo hilo la asakari wetu mutusaidie kwa hilo…makazi ya uhakika ya Polisi yatasaidia kuleta ufanisi “ alisisitiza.

Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania David Mayunga alisema wametoa msaada huo ili kuunga mkono kampeni za Mkoa wa Tabora za kukabiliana na mimba za utotoni, utoro na uimarishaji wa afya kwa wananchi kupitia ujenzi wa Wodi za kinamama.

Alisema mifuko 200 ya saruji itatumika kujenga Wodi katika Wilaya ya Kaliua kwa ajili ya akinamama ikiwa ni kuunga mkono juhudi za kuimarisha afya ya mama na mtoto.

Mifuko iliyobaki itapelekwa katika wilaya za Sikonge , Urambo, Uyui, na  Manispaa ya Tabora ambapo kila moja itapewa mifuko 100 kwa ajili ya kusaidia  kujenga hosteli kwa ajili ya watoto wa kike ili kuunga mkono juhudi za Mkoa za kupambana na mimba mashule zinazotokana na watoto hao kukosa nyumba za kuishi na hivyo kutembea umbali mrefu ambao wakati mwingine ni hatari.

Mayunga alisema pia msaada huo utasaidia kupunguza utoro unatokana na kutembea umbali mrefu kutoka wanapoishi hadi shule na kuwafanya waishi maeneo ya shule.

Aidha kuhusu suala la ujenzi wa nyumba za Polisi alisema wataangali jinsi ya kusaidia kupunguza tatizo hilo baada ya kuwalisialiana na  Makao Makuu ili kuona wanaweza kujenga nyumba ngapi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema msaada huo wa mifuko 200 ya saruji umewaongezea nguvu kwenye ujenzi unaoendelea wa  Hospitali yao ya Wilaya na kuongeza kuwaomba wadau wengine kuwasaidia kwani bado wanahitaji nguvu zao kwa ajili ya kukamilisha mapema ili wananchi waondokane na tatizo la kusafiri umbali mrefu kupata huduma wanapopata rufaa.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora –Uyui Said Ntahondi (wa pili kutoka kulia) jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania. Wengine ni wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mko wa Tabora na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa ampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania David Mayunga.
 Kaimu Katibu  Tawala  Mkoa wa Tabora Ignace Mujwahuzi akitoa maelezo mafupi  jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji wa ampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania David Mayunga akitoa maelezo mafupi  jana kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 600 ya Saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za watoto wa kike na Wodi ya Wakinamama.
  Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Abel Busalama  akitoa maelezo mafupi  jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
 Katibu  Tawala  Wilaya ya  Tabora Sweetbert  Nkuba akitoa maelezo mafupi  jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui Said Ntahondi akitoa maelezo mafupi  jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi  jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shilingi 10.8   kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akishirikiana na viongozi mbalimbali kupokea  msaada jana wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad