HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 22 July 2018

VYUO VIKUU VIZALISHE WAHITIMU WENYE SIFA YA KUTUMIKA KATIKA UCHUMI WA VIWANDA –OLE NASHA

 Naibu Waziri wa Elimu wa Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza katika ufungaji  Maonesho ya Vyuo vikuu nchini pamoja na vya nje vinavyoshiriki maonesho hayo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Salaam.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) Profesa Chareles Kihampa akizungumza wakati ufungaji maonesho kuhusina na uratibu wa maonesho yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu, Habari na Mawasiliano  wa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Omega Ngole wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la bodi  katika maonesho ya vyuo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha  akipata maelezo kutoka kwa  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Umma wa Taasisi ya Uhasibu Nchini (TIA) Lilian Rugaitika wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TIA katika maonesho ya 13 ya  vyuo Vikuu yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha  akizungumza katika banda la bodi ya mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu wakati alipotembelea maonesho ya 13 ya  vyuo Vikuu yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mifumo wa  wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Lameck akitoa maelezo kwa m wananchi aliyetotembelea banda la bodi ya bodi ya mikopo katika  maonesho ya 13 ya  vyuo Vikuu yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU wa Waziri ya Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, amesema kuwa vyuo vya elimu vizalishe wahitimu  wenye sifa ambao watakuwa mchango katika uchumi wa viwanda kwa vilivyopo na vitakavyoanzishwa.

Serikali haitegemei watalaam kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha viwanda wakati vyuo vipo na vinazalisha watihimu kila siku.

Ole Nasha aliyasema hayo wakati akifunga maonesho ya 13 ya vyuo vikuu nchini na Nje ya Nchi yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika vyuo hivyo vinatakiwa kuwaandaa vijana ili waweze kupata stadi na ujuzi stahiki na isiwe bora elimu bali elimu bora kwa nia ya kuelekea uchumi wa viwanda kutokana na dhamira ya serikali ya awamu ya tano chini Dk. John Pombe Magufuli.

Naibu  Waziri huyo, amesema serikali haitavumilia taasisi au mtu yoyote anayejaribu kukiuka miongozo ya uanzishaji wa vyuo visivyo na ubora hatabaki salama ni bora kuwa na vyuo vichache vyenye sifa stahiki na koundoa utitili wa vyuo ambao havina ubora.

‘’Nitoe msisitizo kwa taasisi zote za elimu ya juu ambazo zilihakikiwa na kubainika kuwa zina mapungufu mbalimbali zijirekebishe kasoro hizo mapema iwezekanavyo kwa kuzingatia maelekezo ya Mamlaka husika zinazosimamia ubora wa elimu ya juu, yaani Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE),’’alisema.

Amesema serikali ina mategemeo makubwa ya kupata wahitimu wenye ujuzi unaotakiwa kwenye uchumi wa viwanda.

Mwenyekiti wa Bodi  wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Jacob Mtabaji, amesema maonyesho hayo yamewafanya kukutana na taasisi mbalimbali ambazo simewasaidia kubadilishana uzoefu.

Profesa Mtabaji, amesema maonyesho haya wanategemea kupata wahitimu wenye maadili mema na mahitaji  ambao ni halisi kwa soko.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad