HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 13, 2018

UWT TEMEKE WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA NDEGE YA NNE BOEING 787-8 DREAMLINER

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
JUMUIYA ya Umoja  wa Wanawake  Tanzania (UWT) Wilaya ya Temeke wamempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufulu kwa kuweza kutekeleza ahadi ya kununua ndege ya nne kati ya saba alizoziahidi.

UWT Temeke wamesema kuwa hiyo ni moja ya ahadi zilizoanishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi na wamemuomba aweze kutimiza ahadi zote ili kuhakikisha upinzani wanakosa la kusema.

Akizungumza na wajumbe wa UWT Wilaya ya Temeke, Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi  amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Chama cha Mapinduzi imedhamiria kutimiza ahadi zote zilizoanishwa wakati wa kampeni  na tayari zinafanyiwa kazi ikiwemo kununua ndege ya nne kati ya saba na zile zitakazoanza kutekelezwa kwenye bajeti ya 2018/19.

"Rais wetu Dkt Magufuli aliahidi kununua ndege saba zitakazokuwa mali yetu na mpaka sasa ameshanunua ndege  ikiwemo Boeing  787-8 Dreamliner  na kutimiza idadi ya ndege nne kati ya saba alizotoa ahadi kwenye kampeni zake mwaka 2015,"amesema Mb Mariam.

Mb. Mariam amesema kuwa kwa upande wa Wilaya ya Temeke tayari utekelezaji wa mradi wa barabara, elimi, afya, maji na huduma zinginezo za kijamii pamoja na mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa katika jamii.

Amesema, UWT inatoa rai kwa wananchi wote kwa kumuunga Mkono Rais Magufuli na kujivunia utanzania wetu.

Naye Mwenyekiti wa UWT Temeke Rukia Kamal amemshukuru Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi kwa kuweza kuungana nao katika kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutimiza ahadi ya kununua ndege nne kati ya saba.

Rukia amesema, mbali na hilo Serikali ya awamu ya tano imekuwa inafanya kazi ya kuleta maendeleo kwenye Kata zote  bila kujali chama kwani daima maendeleo hayana chama.

Wanawake wa Umoja huo kupitia kwa Katibu wa UWT Temeke Kimenta Mavala  kwa pamoja waliweza kutoa tamko la kumuunga mkono na kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa maendeleo anayowaletea wananchi wote na kusema wameshaanza kujipanga kwa uchaguzi  wa mwaka 2019 wa Serikali za mitaa na watahakikisha kata zote zilizo chini ya upinzani zinarejea CCM. 
Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi  akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Wilaya ya Temeke wakati wa hafka yao ya kumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Temeke, Rukia Kamal akizungumza na wajumbe wa UWT Temeke wakati wa hafla ya kumpongeza  Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.

Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Temeke Kimenta Mavala akielezea jambo mbele ya wajumbe na Mgeni rasmi wa hafla yakumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.
 Wajumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT)  Wilaya ya Temeke wakiwa katika hafla ya kumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.
 Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe  wa UWT Wilaya ya Temeke wakati wa hafla ya kumpongeza  Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad