HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 4 July 2018

TFDA YAWAALIKA WENYE DHAMIRA YA KUANZISHA VIWANDA KUPATA USHAURI KATIKA MSIMU WA SABASABA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewaalika watanzania wenye dhamira ya kuanzisha viwanda nchini kutembelea banda lao katika msimu huu wa sabasaba ili kupata msaada na miongozo kutoka katika mamlaka hiyo.

Akizungumza na Michuzi blog Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza ameeleza kuwa katika msimu huu wa sabasaba wanasherekea mafanikio ya mamlaka hiyo kwa miaka 15, kuanzia 2003 hadi  2018 na katika kusherekea mafanikio hayo wanatoa elimu mbalimbali katika kuhakikisha uelewa kuhusiana na mamlaka hiyo unakua zaidi.

Bi. Simwanza ameeleza kuwa kama mamlaka wanatoa mwaliko kwa wanaotaka kuanzisha viwanda nchini katika kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ya kuimarisha uchumi wa nchi kama mamlaka watatoa miongozo na elimu kwa wananchi wote watakaotaka kuanzisha viwanda nchini na kuwapatia miongozo ya kufikia malengo yao kwa viwanda watakavyoanzisha vikiwemo viwanda vya vyakula, dawa na vifaa tiba.

Akieleza kuhusiana na mafanikio ya mamlaka hiyo Simwanza ameeleza kuwa wananchi wamekuwa na uelewa kuhusiana na bidhaa ambazo zimepigwa marufuku na mamlaka hiyo na bado wanajitahidi kuhamasisha katika kutoa elimu zaidi.

Aidha ameeleza kuwa kama mamlaka wataendelea na shughuli ya kudhibiti bidhaa ambazo si faafu kwa matumizi ya binadamu na elimu kuhusiana na bidhaa wanazozisimamia itaendelea.

Simwanza ametoa wito kwa wananchi wote kutumia bidhaa zilizoainishwa na mamlaka hiyo na kutoa taarifa pindi waonapo biashara ambazo zimepigwa marufuku na mamlaka hiyo zikiuzwa na kutangazwa kwa kupiga bure 0800 110 084.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza akifafanua jambo mbele ya mkemia mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafumiko mara baada ya kutembelea banda lao la sabasaba.
Mkemia mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafumiko (kushoto)  akizungumza,Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza alipotembelea katika maonesho ya kimata ya sabasaba jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza akionyesha baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku leo katika banda lao la sabasaba alipokuwa akifanya mahojiano na Michuzi blog.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad