HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 19 July 2018

TCRA YAWAWEKA KIKAANGONI HAMISA MOBETO, IRENE UWOYA


*Ni baada ya kuonesha picha zao za hovyo katika Instagramu zao

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WASANII Irene Uwoya na Hamisa Mobeto wamejikuta wakiwekwa kikaangoni na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) baada ya kuweka picha ambazo hazina maadili kwenye Instagramu zao.
Kwa mujibu wa TRCA ni kwamba Uwoya na Hamisa kila mmoja kwa wakati wake waliweka picha ambazo hazistahili na hivyo wameitwa kwa ajili ya kujieleza.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA Valerie Msoka amesema waigizaji hao wamekiuka kanuni ya maudhui inayomtaka msanii kuhakikisha maudhui anayoweka mtandaoni yanakuwa salama na hayamuumizi mtu.

Amesema Hamisa aliweka picha hizo Juni 23 na Uwoya aliweka picha Julai 17 mwaka huu na kwamba baada ya wasaini kuweka picha hizo kamati yao iliwaita ili wajieleze kwani wasichukuliwe hatua.
Ameongeza baada ya kuwasiliza wote wawili wamekiri kosa na kuomba radhi  huku wakiahidi kutorudia tena kufanya kosa la aina hiyo.
"Baada ya kuwasikiliza kamati ilitoa onyo kwa waigizaji hao kwani wakirudia hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kuwataka kuomba radhi katika kurasa zao za instagramu kwa lengo la kuwaelimisha mashabiki wao,"amesema.

UWOYA AISHAURI SERIKALI

Kutokana na onyo la TCRA, Uwoya ametoa ushauri kwa TCRA kutenga siku maalumu kwa ajili ya kutoa semina kwa wasanii wote nchini kwani si wote wenye kuelewa kuhusu kanuni za maudhui mtandaoni.

ALICHOSEMA HAMISA

Kwa upande wake Hamisa yeye amesema hatarudia tena kufanya kosa la aina hiyo huku akitoa ahadi ya kuwa balozi kwa wengine katika kuhakikisha wanaitumia vizuri mitandao ya kijamii na si vinginevyo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad