HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 30, 2018

TBC, UNESCO na EU wazindua studio ya Urithi

Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Utangazaji Nchini (TBC) limezindua studio kubwa ya Kumbukumbu ya ukombozi wa Afrika ya Mwalimu Nyerere katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.
Studio hiyo yenye kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika kanda za sauti na video imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.
Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.
Studio hiyo ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa hifadhi ya mambo ya urithi (TAHAP) wenye lengo la kuhamasisha hifadhi na utunzaji wa urithi wa Tanzania na kumbukumbu za mapambano ya ukombozi katika bara la Afrika, pia itaongeza uelewa wa watanzania juu ya urithi wao ambao umekuwa ukiongezeka jinsi miaka inavyozidi kusonga mbele.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali Dk. Hassan Abbas alisema kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kwamba urithi wa nchi hii unahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi kijacho.
"Kwa sasa tunaondoka katika mfumo wa maandiko, sauti na video.  Sisi kama serikali tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba matukio yetu ya kihistoria yanarekodiwa na kuhifadhiwa vyema. Hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa historia kwa watu wetu na serikali kwa ujumla," alisema Dk Abbas .
Ofisa ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart katika uzinduzi huo alisema kwamba Tanzania ilifanyakazi kubwa ya kusaidia vyama vya ukombozi barani Afrika na kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa mtu muhimu katika harakati hizo zilizolenga kuleta amani, uhuru na umoja wa Afrika.
Alisema sauti na video zinazohifadhiwa katika studio hiyo zitaweza kutumiwa na wananchi kujua historia yao, kujitambua na kuona kazi kubwa iliyofanywa na watu waliowatangulia ili kujua hali ya sasa na kujipanga kwa mambo ya baadae.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk Ayub Rioba, alisema kwamba studio hiyo inayotambulika kama Mwalimu Nyerere African Liberation Memorial Studio itasaidia taifa kuhifadhi kumbukumbu zake katika hali bora zaidi ikiwa ni urithi kwa kizazi kijacho.
"Kwa kutumia rekodi za sauti na video tunaanza kuhifadhi matukio yetu ya kihistoria tangu uhuru. Tunajisikia fahari kuwa chombo ambacho kinatumika kuhifadhi matukio yetu ya kihistoria kwa njia ya sauti na video” alisema.
Mkuu wa Unesco kanda ya Afrika Mashariki, Bi Ann Therese Ndong-Jatta,  amesema kwamba studio hiyo ni moja ya chombo adhimu cha urithi katika taifa ambalo lilitumika sana katika mapambano ya uhuru ikitumia redio yake hasa stesheni ya nje kusaidia harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.
Taasisi za kitaifa zinazohusika na studio hiyo ni pamoja na TBC, Makumbusho ya Taifa, Wakala wa taifa wa hifadhi na kumbukumbu na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Foundation) ambayo inashirikiana na Mradi wa kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika ulipo katika Wizara Ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo.
  Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.

  Mwakilishi wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Tanzania na Afrika Mashariki  Bw. Charlie Stuart akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini.
  Mkurugenzi  na Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. . Ann Therese Ndong-Jatta (kushoto) akipomgezwa na Mkurugenzi  wa Idara ya Habari na Maelezo  na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassani Abasi  wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika katika Shirika la utangazajiTanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utagazaji la Taifa (TBC) Ayub Rioba.
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo na msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la utangazajiTanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini.
 Mkurugenzi Mwakilishi  Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO, Bi. Anna Therese Ndong-Jatta (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba nyaraka za vifaa vya utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU)nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na  Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.
 Kutoka Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Bw. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw.Charlie Stuart, Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi.Anna Therese Ndong-Jatta, ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO Kwa kushirikiana na wadau wa mradi wa Umoja wa Ulaya.(EU)
 Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba  moja ya  Camera pamoja na vifaa mbalilmbali vya utangazaji vilivyotolewa msaada na  UNESCO kwa kushirikiana na wadua na Washirika wa Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini. Kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart.
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na  Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas (wapili kulia) akishuhudia Mkurugenzi Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba moja ya  Kamera pamoja na  vifaa  mbalilmbali vya utangazaji vilivyotolewa msaada na  UNESCO kwa kushirikiana na wadua na Washirika wa Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas (wa pili kulia) akishuhudia Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart akimkabidhi moja ya kifaa cha kurekodia  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba  kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na  Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas (wa pili kulia) akishuhudia Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart akimkabidhi moja ya kifaa cha kurekodia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la utangazajiTanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na  Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas (katikati) akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez akimkabidhi moja ya kifaa cha kuhifadhia kumbukumbu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari  na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,Dkt. Hassan Abbas (katikati)  akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi  mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Ms.Anna Therese Ndong-Jatta(kulia) wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart  na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta, (wa tatu kulia) Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart (kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, wakimsikilza kwa makini mmoja wa wafanyakazi wa TBC akiwaonyesha moja ya mitambo iliyotumika kurekodia enzi kupigania ukombozi wa Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad