HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 10 July 2018

TAMASHA LA NGOMA DANCE LA TULIA TRUST KUSHIRIKISHA MIKOA YOTE TANZANIA BARA, VISIWANI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TULIA Trust waandaaji wa mashindano ya ngoma za jadi nchini wenye kauli mbiu ya "Tuuenzi Utamaduni Wetu" wanataraji kuanza mchakato wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 wakihusisha mikoa yote nchini na visiwani Zanzibar.

Akizungumza na vyombo vya habari Mratibu wa mashindano hayo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameeleza kuwa wako tayari kwa ajili ya mchakato huo  utakaofanyika kuanzia Septemba 20 mpaka 22 mwaka huu huko Rungwe- Tukuyu mkoani Mbeya.

Ameeleza  lengo la mashindano hayo ni kuuenzi utamaduni wetu na kuonesha dunia wana utamamaduni wao na wameanza katika ngoma za jadi ila wataenda mbali zaidi katika  nyanja nyinginezo kama vile lugha, chakula na mavazi.

Aidha ameeleza kuwa wanashirikiana na Serikali katika kupunguza umaskini, hivyo walengwa waone ngoma ni  kazi ambayo itawaongezea kipato, ameeleza kuwa kwa mwaka huu wamelenga kuwa na vikundi 108 vitakavyokutanisha washiriki takribani 2200 ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo vikundi 63 vilihusishwa na 2017 kulikuwa na vikundi 89 na washindi walipewa zawadi mbalimbali kama vile fedha taslimu, pikipiki na ile ya kuendelezwa kimasomo katika chuo cha Sanaa Bagamoyo katika ngazi mbalimbali na hadi kufikia sasa takribani washiriki 30 wamepata fursa hiyo.

Kuhusu mafanikio  Dk.Tulia ameeleza kuwa washiriki watapata zawadi mbalimbali na kuwezeshwa zaidi, na amesema kuwa hadi sasa wana mkataba na hoteli za kitalii ambazo ngoma za jadi hutumbuiza na mafanikio yaliyotia moyo zaidi ni yale ya kikundi cha Bujora dance kutoka jijini Mwanza kuwakilisha taifa nchini India katika miji 3 na kurudi na ngao ya  ushindi nchini.

Kuhusu utaratibu wa kuwapata washiriki hao Dkt Tulia ameeleza kuwa watashirikiana  na maafisa utamaduni kote nchini katika mchakato wa kupata washindi hao aidha ametoa wito kwa makampuni ya simu kuwasaidia wananchi hao kupitia nyimbo zao ili waweze kupata kipato.
Mratibu wa Tamasha la Tulia Trust Dance Festival Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo litakalofanyika Septemba 20 hadi 22 Rungwe Tukuyu Mbeya Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad