HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 12, 2018

TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA KUFANYIKA JUMAMOSI

Na Mwandishi Wetu,
TAMASHA la Majimaji Selebuka linalohusisha mashindano ya  mbio za baiskeli, riadha, ngoma za asili na Midahalo kwa wanafunzi wa shule  mbalimbali za Sekondari katika  Manispaa ya Songea mkoani RuvumaTamasha hilo linatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa  michezo wa Majimaji mjini Songea.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, mtaratibu wa Tamasha hilo Osam Ulaya alisema tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti na matamasha mengine yaliyowahi kufanyika hapo awali.

Kwa mujibu wa Osama, Tamasha la mwaka huu litashirikisha pia vikundi vya ngoma vya asili kutoka mkoa jirani wa Mbeya,  ambavyo vitashindana na vikundi vya ngoma vilivyopo katika  manispaa ya Songea kwa lengo la kuleta hamasa na litasaidia sana kuinua kipato kwa wananchi wa manispaa  ya Songea, ambao watatumia fursa hiyo kufanya Biashara na wageni watakao udhuria.

Ulaya alisema, pia Tamasha la Mwaka huu wameongeza kipengele cha Ujasiriamali ambapo zaidi ya vikundi 10 tayari vimeshathibitisha kushiriki, sambamba na washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Hata hivyo Ulaya alisema, Tamasha la 2018 linatarajiwa kuhudhuriwa na  Balozi wa Norway na Balozi wa Poland hapa nchini ambao wamependa kushiriki Tamasha hilo ambalo litakuwa chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Songea na mkoa wa Ruvuma.

Aidha alisema,  Mdahalo wa mwaka huu utafanyika kwa lugha ya Kiswahili badala ya Kiingereza ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuonesha uwezo wao katika matumizi ya lugha ya Taifa na namna wanavyoielewea  vizuri wilaya ya Songea ambayo ina fursa nyingi ambazo bado hazifanyiwa kazi.

Alisema, katika Tamasha hilo washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na washindi wa kwanza hadi wa tatu katika  mchezo wa riadha watapata nafasi ya kwenda Nchini Afrika Kusini kushiriki mbio za Marathon.
Kwa upande wake, Godfre Mvulla ambaye ni  katibu wa Chama cha Mpira wa miguu Manispaa ya Songea(SUFA)alisema, katika Tamasha la Mwaka huu wachezaji wa  zamani wa Timu  za Simba na Yanga watashiriki kwa kucheza mchezo maalum.

Mvulla alisema, mchezo huo ambao utaonesha na kituo cha Azam Tv na utatangazwa  na watangazaji nguli Charles Hilary na Sued Mwingi na kiingilio katika mchezo huo itakuwa shilingi 2000 ambayo itamwezesha kila mwanachi kuhudhurioa mchezo huo.
Mratibu wa Tamasha la Majimaji Selebuka Sam Ulaya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mjini Songea kuhusiana na maandalizi ya Tamasha hilo linalo tarajiwa kufunguliwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Michezo wa Majimaji mjini Songea. Katikati ni katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu katika  Manispaa ya Songea,  God Mvulla na Kulia mwamuzi mstaafu Mary Kapinga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad