HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 12 July 2018

TaGLA YAENDELEA NA MAFUNZO YA UPANGAJI MIJI, YAJADILI MASUALA YA ELIMU NA MIUNDOMBINU

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAKALA wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) wameendelea na mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi wa wakala hiyo Charles Senkondo ameeleza kuwa huo ni mdahalo wa pili kati ya saba inayotarajiwa kufanyika hadi kufikia oktoba mwaka huu,  na katika mdahalo huo wamejifunza uwiano wa majiji na utofauti wake kimaisha na hii husaidia kupata takwimu za uhalisia wa maisha katika majiji mbalimbali.

Senkondo ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatolewa na profesa Heungsuk Choi kutoka chuo cha maendeleo cha korea kusini katika kueleza namna ya upangaji wa miji na majiji kisasa na kuzingatia miundombinu iliyo bora zaidi ambayo husaidia wananchi katika shughuli zao za kimaendeleo kama vile biashara na hata kirahisisha usafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Aidha ameeleza kuwa katika mdahalo huo suala la elimu limejadiliwa na imeelezwa kuwa mazingira ya upatikanaji wa elimu lazima yaboreshwe kwani wazazi huwapeleka wanafunzi katika shule bora zaidi, hivyo shule ambazo hazina ushawishi ni vyema zikaboreshwa zaidi.

Pia Senkondo amewaomba wadau wa serikali na taasisi binafsi kuitumia wakala hiyo ili kuweza kushirikiana na Serikali katika kujenga miji na majiji.

Pia mdau wa mazingira ambaye pia ni mkurugenzi wa Legendary International Limited Kamugenyi Luteganya,  ameeleza kuwa semina hiyo ni muhimu sana katika jamii katika kuishi mazingira yaliyo bora na safi kama Korea wanavyofanya na kuboresha kwa kila hatua hivyo ni lazima wachukue ujuzi ili kuweza kuboresha makazi  nchini.

Pia ameeleza kuwa Serikali na sekta binafsi kutia mkazo katika suala la mazingira na kutoa elimu, na hii ni sambamba na kutoa sera mikakati juu ya upangaji na matumizi ya ardhi.

Washiriki wa mjadala huo wamewashauri wadau na wananchi kwa ujumla kishiriki katika midahalo hiyo ili kuweza kujifunza namna ya kuboresha na kujua uhalisia dunia inavyoshiriana katika kukuza na kujenga miji na majiji duniani.
 Mkurugenzi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Charles Senkondo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.
Mkurugenzi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Charles Senkondo  na wadau wengine wakifutialia mdahalo mubashara toka Nchini Korea Kusini.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad