HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 24 July 2018

RAIS WA TFF AFAFANUA ONGEZEKO LA WACHEZAJI WA KIGENI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia amesema kuwa ongezeko la wachezaji kumi wa kigeni ni makubaliano baina ya timu husika za ligi na bodi ya ligi.

Karia ameyasema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ongezeko hilo na kusema kuwa klabu zenyewe ndiyo zilizopendekeza kuongeza wachezaji kutoka saba hadi kumi.

Karia amefanya hivyo baada ya wadau akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe kutoa maoni ya kupinga uamuzi huo uliochukuliwa na TFF.

Karia amesema klabu za ligi kuu kupitia kwa aliyekuwa mwenyekiti wao wa bodi ya ligi (Clement Sanga) walikutana katika kikao cha Tarehe 30 juni 2018 katika ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa kuzungumzia masuala kadhaa likiwemo suala la kanuni mpya za ligi kuu.

"Viongozi wa klabu pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ua Ligi walikutana katika kikao kilichokuwa kinazungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya kanuni mpya za ligi kuu na katika hayo pia waliweza kujadili ongezeko la wachezaji kutoka saba mpaka kumi na wakafikia makubaliano ya pamoja,"amesema Karia.

 Karia ameongeza klabu zenyewe ndiyo zilipendekeza ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka saba mpaka wachezaji 10. Mapendekezo ya Kanuni yalijadiliwa katika Kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF na wakakubaliana na hoja za ongezeko hilo katika Ligi kuu na kupitisha maombi yao.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad