HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 8, 2018

RAIS MSTAAFU KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA 42 YA KIMATAIFA YA BIASHARA

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) akimsikiliza Naibu Mpambe wa Bunge, Ndg. Peter Magati akimfafanulia kuhusu historia ya Bunge na Baadhi ya majengo yaliyotumiwa na Bunge kuanzia kipindi cha ukoloni, baada ya kupata uhuru mpaka sasa wakati alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea leo tarehe 8 Julai, 2018 katika Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.  
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea leo tarehe 8 Julai, 2018 katika Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea leo tarehe 8 Julai, 2018 katika Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Eng. Stella Manyanya na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndg. Edwin Rutageruka
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ofisi ya Bunge alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea leo tarehe 8 Julai, 2018 katika Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Eng. Stella Manyanya na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndg. Edwin Rutageruka

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad