HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 18, 2018

MRADI WA MAJI WA KIMBIJI NA MPERA UTASAIDIA UPATIKANAJI WA LITA MIL 260 KWA SIKU-PROF MBARAWA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ametembelea mradi wa uchimbaji wa visima virefu vya Kimbijii na Mpera wenye thamani ya Bilioni 19.6  vitakavyosaidia kupatikana kwa lita za maji Milioni 260 kwa siku.

Mradi huo wa visima vya maji uliochini ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) una lengo la kuongeza wingi wa maji katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na kufikia lita Milioni 720 kwa siku kufikia mwaka 2032.

Prof Mbarawa akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA  Dkt Suphian Masasi ameweza kukagua visima hivyo na kuwataka wakandarasi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kukagua visina hivyo, Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo utawasaidia wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwa utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama na yatakayotosheleza kwa matumizi yao.

" Mradi huu wa Kimbiji na Mpera utakaotoa Lita Milioni 260 kwa siku utasaidia sana wananchi wa Dar es Salaam, ukichukulia Mradi wa Ruvu Juu na Ruvu chini unatoa lita Milioni 502 kwa siku kwa ujumla wake utaleta chachu ksa wananchi kupata maji kwa uhakika,"amesema Prof Mbarawa.

Amesema kuwa, kukamilika kwa visima hivi kutaimarisha upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo hayakuwa na huduma nzuri ya majisafi na yale yasiyo na mtandao rasmi.

Prof Mbarawa akitoa maagizo mbele ya Mkurugenzi Wa DAWASA, ameitaka kampuni ya Serengeti ya nchini Tanzania na Mkandarasi kutoka kampuni ya NSPT ya nchini Iran kuhakikisha mradi huu unaenda na muda ulipangwa kwakuwa tayari umesuasua   kwa mrefu haujamalizika.

" Kampuni yenu naipa wiki moja kwanza wawasilishe malipo ya bima kwa wafanyakazi, vifaa pamoja visima vyenyewe ambapo gharama yake haizidi hata Bilioni 4  na mkishafanya hivyo mniletee nione," 

Kwa upande wa DAWASA, Kaimu Mkurugenzi  Dkt Suphian Masasi amesema kuwa wanategemea mradi huu uende kwa haraka zaidi ili wananchi wapate maji ambapo wameona kuna baadhi ya maeneo wataamua kuyafanya wao kama Mamlaka husika kama ununuaji wa vifaa, kuwalipa baadhi ya watendaji moja kwa moja ili kuweza kurahisha umalizikaji wa kazi ili watu wapate maji.

"Sisi tunafuata maagizo ya Waziri kwahiyo kinachofuata ni utendaji tu na kuna maeneo tutawekea tija ikiwemo kuwalipa watendaji yawekezna ipo changamoto ya ulipaji kwa wakati pia hata ununuaji wa vifaa tutafanya hivyo pale inapohitajika na kisha baadae tutawakata katika malipo yao,"amesema Dkt Masasi.

Naye Msimamizi wa miradi ya Maji kutoka kampuni ya Dkt Charles Kaaya amesema kuwa katika utafiti wao wa visima 19 ambavyo tayari vimekamilika wanaimani upatikanaji wa maji utakuwa ni ule ambao umekadiriwa wa lita Milioni 260 kwa siku.

Tayari visima 19 kati ya 20 vya mradi wa Kimbini na Mpera vimekamilika na vina kina kati ya mita 435 hafi 625 huku baadhi vikiwa na uwezo wa kuzalisha lita 100,000 hadi 450,000 kwa saa na mradi huu umetekelezwa na serikali ya Tanzania ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wake wa Dar es Salaam.

Maeneo yatakayonufaika kwa mradio huo ni Kigamboni, Chanika, Chamazi, Pugu, Kibada, Kisarawe 2, Kongowe, Gongo la Mboto, Segerea, Charambe, Buyuni, Mbagala, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Tazara, Ukonga, eneo la viwanda la Barabara ya Nyerere, Mji wa Mkuranga mkoa wa Pwani pamoja na  vitongoji vyake vikiwemo Kisemvule na Kibamba.
WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa miradi ya maji wa kampuni ya EGIS, Dk. Charles Kaaya, kuhusu kupima urefu wa kisima kirefu katika mradi wa maji wa visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.
 WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa  akinywa maji katika moja ya Kisima ya miradi ya maji ya Kimbiji na Mpera wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.
 WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiwa pamoja Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasikatika mradi wa maji wa visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam utakaofanikisha upatikanaji wa lita Milioni 260 kwa siku.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad