HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 11 July 2018

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ATOA MWEZI MMOJA KWA MADEREVA WA BODABODA WOTE KUWA NA LESENI ZA UDEREVA

VICTOR  MASANGU, KIBAHA
MKUU  wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama  ametoa muda wa mwezi mmoja  kwa madereva wote wa pikipiki  kuhakikisha wanakuwa na leseni kwa lengo la kuweza kupunguza na kuondokana na  ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipoteza maisha ya watu na nguvu kazi ya Taifa hususani kwa  vijana hao.

Agizo hilo amelitoa  leo wakati wa mkutano maalumu ambao aliuandaa kwa lengo la kuweza kuwakutanisha na wadau mbalimbali  wa maendeleo ili kuweza kusikiliza kero pamoja na kubaini changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika utekelezaji wa  majukumu yao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Pia  katika hatua nyngine Mkuu huyo alibainisha kuwa  vijana wengine  ambao ni madereva  wa pikipiki katika Wilaya Kibaha wamekuwa wakivunja sheria mbalimbali za barabarani ikiwemo kutokuwa na leseni  hivyo wanahatarisha usalama wa maisha yao pamoja na abiria ambao wanaowapakia kwani kufanya hivyo ni kinyume kabisa na sheria za taratibu za usalama barabarani.

“Kwa kweli kutokana na kuwepo kwa changamoto hii ya madereva wa pikipiki nimeamua kuitisha mkutano kwa ajili ya kuwakutanisha wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na taasisi mbali mbali ili kuwez kujadili kwa pamoja na kuweza kuona namna gani tunaweza kuwasaidia vijana hawa waweze kupata leseni pamoja na kuwezeshwa katika mikopo,”alisema Assumpter.

Nao madereva  hao wa pikipiki wakizungumza katika mkutano huo wamesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kutokuwa na leseni, kofia ngumu pamoja na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala mbalimbali ya sheria za usalama barabarani hivyo kupelekea kusababisha kutokea kwa ajali ambazo zinapoteza  maisha ya watu pamoja na majeruhi.

 Madereva hao akiwemo Ahmad Suleman  na  Said Issa   walisema kwamba kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kutokana na wakati mwingine wanajikuta wanatekwa na watu wasiofahamika kwa kuwawekea madawa ya kulevya na kuwafanyia vitendo vya kikatili  kisha kuwatupa maporini na kuondoka na pikipiki, huku baadhi ya wengine wakipoteza maisha yao.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kuona kero yetu ya siku nyingi ya kuendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na leseni, lakini kwa kutukutanisha na mamlaka zinazohusika tumeweza kupata elimu ya kutosha pamoja na jinsi ya kuweza kupatiwa taratibu zote za kuweza kupata leseni ambayo tutakuwa tunailipia kwa awamu,”walisema madereva hao.

 Naye Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Kibaha Edward Gontako aliwataka kuhakikisha wanazingatia sheria zote za barabarani na kwamba wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kuweza kutoa elimu na mafunzo mbali mbali ya sheria za usalama barabarani lengo ikiwa ni kuweza kupunguza ajali amabzo wakati mwingine zimekuwa zikisababisha na  uzembe  wa baadhi ya  madereva.

Isack Msemwa ni moja na wadau ambao walihudhulia katika mkutano ho ambaye pia msimamiSzi wa utoaji wa mikopo kutoka benki ya CRDB tawi la mbezi Jijini Dar es Salaam  alibainisha kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaweka mikakati kabmbe ya kuwasaidia vijana ambao ni madereva pikipiki kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

WILAYA ya Kibaha Mkoani Pwani kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikibabiliwa na changamoto kubwa ya kuwepo kwa baadhi ya madereva ambao wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto bila ya kuwa na leseni  pamoja na kutovaa kofia ngumu,hali ambayo inahatarisha  kwa kiasi kikubwa usalama maisha yao.                                 
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kufungua mkutano wa madereva wa pikipiki  kwa ajili ya kukutana na wadau kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo kutokuwa na leseni, pamoja na kofia ngumu ili kuweka mikakati ya kuwasaidia pamoja na kupunguza wimbi la ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza.
 Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Kibaha Edward Gontako akizungumza na wanahabari kuhusina na mikakati waliyojiwekea katika kuhakikisha wanapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipelekea kupoteza maisha ya watu(PICHA NA VICTOR MASANGU)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad