HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 2, 2018

MKUTANO WA SITA WA KISAYANSI WA MUHAS WAFUNGULIWA NA WAZIRI NDALICHAKO


Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo amefungua Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam huku akitoa wito kwa taasisi za elimu ya afya na mashirika mbalimbali yanayofanya tafiti za afya hapa nchini kuhakikisha tafiti hizo zinafika kwa wadau na wananchi.

“Kwa sasa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda na miongoni mwa sekta muhimu ambazo pia zinatarajia wawekezaji ni pamoja na sekta ya afya hivyo basi muelekeo na mapendekezo ya tafiti za afya ndio zitakazoweza kuwasaidia wadau na serikali kufahamu aina ya ukwekezaji huo pamoja na maeneo gani yanafaa kulingana na mahitaji.”Alibainisha.

Aliongeza kuwa Serikali kwa kiasi kikubwa inajitahidi kutumia tafiti hizo katika kuandaa sera mbalimbali zinazohusiana na masuala ya afya huku akitoa pongezi kwa uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuandaa wataalamu wanaoandaa tafiti hizo kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Awali, akizungumza kwenye hafla hiyo Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe alisema nyingi kati ya tafiti zitazowasilishwa kwenye mkutano huo wa siku mbili zitajikita katika vipaumbele vya taifa yakiwemo masuala ya HIV/AIDS, kifua kikuu, afya ya uzazi na mtoto, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ajali pamoja na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika.

“Zaidi umuhimu wa mkutano huu ni kuwa unawakutanisha wataalamu wa afya tena katika ngazi tofauti wakiwemo wale waliobobea pamoja na wanafunzi na hivyo kuwa kama jukwaa kwa wao kuweza kubadilishana ujuzi. Zaidi ya tafiti tofauti 200 zitawasilishwa kupitia mkutano huu’’ alisema.

Aliishukuru serikali ya Sweden kupitia Shirika la Sida ambao kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha mkutano huo
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati akifungua mkutano huo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad