HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 9 July 2018

MBUNGE WA MANONGA AZINDUA MADARASA NA MABWENI KWA AJILI KIDATO CHA TANO NA SITA

Na Ripota wetu
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali amezindua rasmi madarasa 2 na mabweni 3 yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

Gulamali ameeleza kuwa huo ni moja kati ya miradi ya kimaendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika jimbo hilo na amefurahi kuzindua mradi huo ambao utawasaidia wanafunzi wengi kutimiza ndoto zao kielimu.

Aidha ameeleza kuwa miradi ya kimaendeleo katika sekta ya afya, Umeme, elimu na miundombinu ni muhimu kwa wananchi katika kuleta maendeleo hivyo kama serikali hawana budi kuipa kipaumbele. Katika mwaka huu wa fedha, vijiji vyote katika jimbo la Manonga vitapata umeme na tayari  Mbunge huyo ameshatekeleza ahadi yake kwa kukabidhi gari jipya la wagonjwa jimboni humo.

Uzinduzi wa madarasa na mabweni hayo utawasaidia wanafunzi kujiunga na elimu ya kidato cha tano Mkoani humo na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekondari ya juu kutokana na uhaba wa shule. 

Katika uzinduzi huo Gulamali aliambatana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka WCB wakiongozwa na Lavalava pamoja na Maromboso walioambatana na jopo la timu yao.
 Mbunge wa Manonga (kushoto) Seif Gulamali akikabidhi vifaa vya shule kwa mmoja wa wanafunzi wakati wa uzinduzi wa madarasa 2 na mabweni 3 yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii na baadhi wa wanafunzi wa sekondari Ziba. 
Mradi wa madarasa 2 na mabweni 3 yaliyozinduliwa na mbunge wa Manonga yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad