HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 17 July 2018

ACACIA WATOA MSAADA WA SHILINGI MIL NANE KWA ATFGM MASANGA TARIME

Na Frankius Cleophace Tarime
KAMPUNI ya uchimbaji wa mawe yenye dhahabu ya Acacia North Mara wametoa msaada wenye thamani zaidi ya Sh.milioni nane katika Kituo cha kuifadhi wahanga wa ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji cha ATFGM Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.

Akisoma risala Meneja Miradi Shirika la Associatio for the Termination of Female Genital Mutilation ATFGM Masanga Valerian Mgani ametoa shukrani kwa niaba ya shirika hilo na kufafanua vifaa vilivyotolewa vina thamani ya Sh. 8,823,000 kwa lengo la kusaidia mabiti ambao watapokelewa kipindi cha Kambi Desemba mwaka huu.

"Kwani huenda ukeketeaji ukawepo licha ya wazee wa vila kupiga vita,"amefafanua.Pia mbali na watoto hao kukimbia ukeketaji uenda katika kituo hicho kwa ajili ya kupata elimu ya makuzi, hivyo mahitaji na kwamba msada uliotolewa una muhimu mkubwa.

Vitu vilivyotolewa na ACACIA ni Godoro 20, shuka 100,shuka za imasai 100, blanketi 100, taulo za kike(pedi) 1000,sabuni katoni 300, mafuta kopo187 na vitu vingine kadhaa.Pia Meneja huyo ameiomba Kampuni ya ACACIA kusaidia kujenga nyumba za wafanyakazi na wahanga wa matukio hiyo ambapo amesema fedha zinazohitajika ni Sh.488,804,400.

Huku akieleza mafanikio yao tangu kuanzisha kambi hiyo na suala la kutoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike ambapo wameokoa mabinti wengi.Ameongeza pia wamepeleka shule mabinti 102 shule ambao wamekataliwa na wazazi wao kwasababu walikataa kukeketwa na kuunga vikundi kwa Mangariba waliacha kukeketa na kuendelea kutoa elimu hiyo.

Kwa upande wa Kaimu Ofisa Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya ACACIA North Mara Reuben Ngusaru amesema maombi yote yamepokelewa na atayafikisha kwa wahuska ili kuyafanyia kazi.Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya ameiomba Serikali kuchukua hatua kali kwa wale watakaobanika kukeketa mtoto wa kike.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Muriba Kaleb Fanuel aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga amesema upendo, mshikamano ndio kitu cha muhimu katika kutomeza mila na desturi ambazo zinamkandamiza na kumumiza mtoto wa kike.

Aidha baadhi ya mabinti ambao ni wahanga wa matukio hayo ambao kwa sasa wanalelewa na kituo hicho wanazidi kuomba Serikali sasa kuchukua hatua kali kwa wazazi, walezi ambao wanawatenga kisa wamekimbia ukeketaji.

  Mkurugenzi wa Ushirika wa ATFGM Masana Sister Stella Mgaya akiongea katika hafla hiyo fupi ambapo ameiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wale ambao watakeketa Mwaka huu.
 Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga Valerian Mgani akitaja mafanikio ya Ushirika huo na kuomba Kampuni ya ACACIA Kusaidia katika ujenzi wa Nyumba za wafanykazi na wahanga wa ukatili kias cha Shilingi488,804,400 ili kukamilisha ujenzi huo.
Kaimu Jamii Endelevu ACACIA Reuben Ngusaru akiongea katika haflya hiyo ya makabidhiano ya msaada huo ambapo amesema maombi lazima ayafikishe kwa Viongozi wake ili kuyafanyia kazi.
Kaleb Fanuel Afisa mtendaji wa kata ya muriba aliyemwakilsha Mkuu wa wilaya ya Tarime Gloriuos Luoga akiongea kwa niaba yake ambapo amesema serikali itaendelea kusimamia sheria.
   Kaimu Jamii Endelevu ACACIA Reuben Ngusaru akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Wasichana hao ambao ni wahanga wa ukatili wa kijinsia Ukiwemo Ukeketaji.
  Mkurugenzi wa Ushirika huo Sister Stella Mgaya akikabidhi vifaa hivyo kwa Mabinti hao.
 Baadhi ya vifaa vilivyotolewa katika Ushirika wa ATFGM Masanga na kampuni ya Uchimbaji wa Mawe ya dhahabu ACACIA North Mara Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad