HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 1 June 2018

Wizara yakabidhiwa jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisaini hati ya kukubali rasmi kupokea jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri kuhusu Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika Mashariki. Kushoto ni Bw.Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye alikabidhi majukumu ya usimamizi wa Bodi hiyo kwa Wizara.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha .

Bodi hii yenye makao makuu yake jijini Arusha, Tanzania, tokea kuanzishwa kwake tarehe 30/01/2013 ilikuwa chini ya uangalizi wa TAKUKURU. 
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakifurahia jambo baada ya kuasaini hati za makabidhiano 
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akipokea nyaraka za Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw.Valentino Mlowola 
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji na Watumishi wa Serikali, na Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad