HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 6 June 2018

WAZIRI MKUU AWASISITIZA WABUNGE WADUMISHE MSHIKAMANO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasisitiza wabunge waendelee kudumisha  mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa nchi tulivu na yenye amani.

Amesema mshikamano na upendo walionao wabunge hao ni vema wakauendeleza ili waweze kutekeleza shughuli zao za kuishauri Serikali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Juni 5, 2018) katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma wakati wa futari aliyowaandalia wabunge. Futari hiyo ilihudhuriwa na wabunge wa vyama vyote.

"Mshikamano na upendo huu tuliouonesha kuanzia mwanzo wa mkutano wa Bunge naomba tuudumishe ili tuweze kuishauri vizuri Serikali na tufikie malengo tuliyojiwekea,” alisema. 

Naye,Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye alitoa neno   la shukurani kwa niaba ya wabunge wote alimshukuru Waziri Mkuu kwa heshima aliyowapa.

"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii heshima uliyotupa ni kubwa, kualikwa na wewe si jambo dogo si kila mtu anaweza kupata nafasi hii," alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mgogoni, Mheshimiwa Dkt. Suleiman Ally Yussuf ambaye alisoma dua alisema watu wanatakiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliowapa.

“Kuna wenzetu tulioshirikiana nao kwenye mfungo wa Ramadhani mwaka uliopita lakini leo hatunao sababu wametangulia mbele ya haki, hivyo sisi tunatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliotupa,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Malindi Zanzibar, Ally Abdullah Saleh, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 5, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, wakati wa futari aliyowaandalia wabunge, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018, kushoto ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, baada ya futari aliyowaandalia, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson, baada ya futari aliyoiandaa kwa wabunge, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad