HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 5 June 2018

WATEJA WA BANKI YA EXIM JIJINI DAR WAFUTURISHWA


 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania, Selemani Ponda akito shukran wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wao wakubwa wa Dar e Salaam jana iliyofanyika katika hoteli ya New Africa.


Mteja wa benki ya Exim Tanzania, Mr Murtaza, akitoa shukrani kwa menejimenti ya benki katika half ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo mwisho wa wiki iliyopita katika hoteli ya New Africa Dar es Salaam. Wateja na wafanyakazi 100 wa benki ya Exim Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.


KATIKA kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhan, Benki ya Exim Tanzania imefuturisha wateja wake wakubwa jijini Dar es Salaam. 
Futari hiyo ilililenga kuleta pamoja wateja na kuthibitisha ahadi ya benki ya kuelewa mahitaji ya wateja hao na kuzidi matarajio yao. Menejimenti ya Benki ya Exim Tanzania pamoja na wateja wake walihudhuria futari hiyo iliyofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim, Selemani Pondaakizungumza wakati wa maandalizi ya futari hiyo alisema, "Tunavyoadhimisha siku hizi za heri za mwezi huu mtukufu, tumeandaa futari hii kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu na kutambua msaada wao endelevu. Katika miaka ishirini ya shughuli zetu, tumeweza kupata sifa ya benki yenye ubunifu na ubora ambazo tusingeweza kufikia bila uaminifu kutoka kwa wateja wetu." Benki itafuturisha wateja wake wakubwa na wadogo katika mkoa wa Tanga, Mtwara na kisiwa cha Zanzibar."

Kwa mujibu wa msemo wa Kundi la Exim, Exim iko kwenye kazi, leo kwa kesho, Benki imeendelea kutekeleza njia mpya za kukidhi mahitaji ya wateja wa makundi yote; kampuni kubwa, wateja wa SME na wateja binafsi kwa hali ya juu. Benki inategemea kuzindua huduma kadhaa za kidijitali kwa mwaka 2018 kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad