HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 June 2018

Watanzania kumjua Mengi kupitia uzinduzi wake wa kitabu kuhusu maisha yake

KUNA maswali mengi sana yanayoulizwa na watu mbalimbali kuhusu mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi, alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu.

Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani.

Ndani ya kitabu hiki ambapo wakali wa tafakari kimataifa wameandikia maelezo yao ya kukiafiki kama kitabu bora kinachostahili hata kufundishia.

Kitabu hicho ambacho kinaelezea safari ya maisha ya Dk. Mengi kutoka kwenye maisha ya kimaskini mpaka kufikia kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa hapa nchini kitafanyiwa uzinduzi Dar es salaam na kinatarajiwa kuwa mwongozo kwa wasomaji, hususan vijana wanaotaka kuwa wajasiriamali.

Kitabu hiki ambacho kinaitwa “I Can, I Will, I Must…The Spirit of Success” (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio”, na kinaelezea kwa undani mambo aliyoyapitia Dk. Mengi mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.

Mambo ambayo yanaelezewa kwenye kitabu hicho yamekuwa yakichambua kiini cha msongo kwani majaribu, matatizo, changamoto pamoja na maeneo aliyoshindwa lakini hakukata tamaa kutokana na nia madhubuti na malengo ya kutaka kufanikiwa.

Mpaka hivi sasa kitabu hicho kimeshapongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, ambaye amekielezea kuwa ni simulizi ya mafanikio ya hali ya juu na ni cha kwanza cha aina yake barani Afrika.

Ameongeza kuwa simulizi ya kitabu hicho imeweza kuelezea kwa ufasaha na kiufundi jinsi mifumo ya kiuchumi na kisiasa iliyokuwa ikibadilika kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio.

Pia kitabu kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profesa Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia.


Kwa taarifa zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake ‘like’ na ‘follow’ akaunti zake za mitandao ya kijamii kupitia twitter @regmengi na instagram @regmengi

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad