HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 7 June 2018

WAHARIRI WAOMBWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA

Na Ripota Wetu
WAHARIRI wa vyombo vya habari nchini wameombwa kushirikiana na serikali katika kila jambo linalohusu sekta ya afya ili kuhakikisha jamii inapata ujumbe sahihi kuhusu sekta hiyo.

Ombi hilo limetolewa na Meneja wa Mapango wa Taifa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Angela Ramadhani, wakati akifunga mafunzo ya siku moja kwa wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali jana jijini Dar es Salaam kuhusu ujio ‘Furaha Yangu’ yenye lengo la kuhamasisha upimaji na utuamiaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.

Dk. Ramadhani alisema vyombo vya habari ni mdau muhimu katika kampeni na kazi abazo wanafanya kila siku hivyo anaamini iwapo ushirikiano utakuwepo juhudi za kukabiliana na maambukizi ya ukwimu zitapata suluhu.

Alisema wameamua kukutana na wahariri ili kuwajengea uwezo wakiamini kuwa ni kiungo muhimu katika kufanikisha mipango mbalimbali ambayo wanatarajia kutekeleza kwa siku za karibuni kupitia NACP na wadau wengine.

“Tumewaita ili kuweza kubadilishana mawazo kuhusu kinachofanyika NACP, ambapo kwa sasa tunatarajia kuzindua kampeni mpya ya ‘Furaha Yangu’ jijini Dodoma.
Alisema NACP kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inajipanga kuhakikisha asilimia 90 ya watu wanaishi na virusi vya ukimwi wanajitambua, 90 ya wanatumia dawa na asilimia 90 ya wenye maambukizi hawaambukizi wengine.

Dk. Ramadhani alisema pia Serikali kwa kushirikiana wadau mbalimbali inatarajia ifikapo mwaka 2030, ukwimu usiwe janga katika jamii ya Kitanzania.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Shoko Subira aliwaomba waandishi na wahariri wa vyombo vya habari kutumia lugha na takwimu sahihi katika habari ambazo wanaripoti ili kuepusha mgongano wa tafsiri.

Subira alisema jamii ya Kitanzania inahitaji kupata taarifa sahihi hivyo ikitokea lugha haijaeleweka inachangia mkanganyiko kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.

Alisema katika kuongeza wigo wa jamii kutambua shughuli zinazofayika katika wizara wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari wakiamini kuwa hiyo ndio njia ya kufikisha taarifa kwa usahihi.

“Pamoja na mambo mengine tunapenda kuwakumbusha kutumia taarifa sahihi hasa katika takwimu kwani kinyume chake kinaleta matatizo katika ofisi,” alisema.

Akizungumzia Kampeni hiyo, Ofisa kutoka Shirika la fhi360, Johnbosco  Basomingera, alisema wamekuja na Mradi wa USAID ‘Tulonge Afya’ wakiamini kuwa ni njia muhimu ya kufanikisha mapambano dhidi ya ukwimu.

Alisema kampeni hiyo ‘Furaha Yangu’ ya kupima na kutumia dawa unatarajia kutoa taarifa ambazo zitakuwa nzuri kwa nchi hasa katika kukabiliana na viruzi vya ukimwi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad