HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 22 June 2018

Timu ya Madaktari Kutoa Hudumza Kitabibu Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Mbeya

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makani Makwaia akikaribisha timu ya wataalamu kutoka China ambao wamekuja kujenga uwezo kwa wataalamu wa hapa nchini na kusaidia maeneo ambayo yana upungu wa wataalamu Muhimbili, Taasisi ya Mifupa MOI, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.  Kutoka kushoto ni viongozi wa watalaamu hao na kulia ni Mkurungezi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi na anayefuatia ni mwakilishi wa MOI, Dkt. Swai. Leo Muhimbili, MOI na JKCI imewaaga wataalamu watatu ambao walikuwa hapa nchini. Tanzania na China imekuwa ikishinikiana kwa zaidi ya miaka 50 katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo sekta ya afya.
 Wataalamu kutoka China ambao watashirikiana na wataalamu wetu wa MNH, MOI, JKCI na Hospitali ta Rufaa ya Mkoa Mbeya katika kutoa huduma za kitabibu. Miongoni mwa kundi hilo wamo wataalamu watatu; Dkt. Zhu Jian, Dkt.Wang Qiang na Song Tao ambao wameagwa leo baada ya kumaliza muda wao.
 Mwakilishi kutoka MOI akizungumza na wataalamu kutoka China
ambao wamekuja kujenga uwezo kwa wataalamu wa hapa nchini na kusaidia maeneo ambayo yana upungu wa wataalamu Muhimbili
 Mkurungezi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akiwakaribisha watalaamu hao kutoka China ambao wamekuja kujenga uwezo kwa wataalamu wa hapa nchini na kusaidia maeneo ambayo yana upungu wa wataalamu Muhimbili
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makani Makwaia akimpatia cheti Dkt. Zhu Jian ambaye amemaliza muda wake.
 Dkt. Wang Qiang akionyesha cheti chake baada ya kupewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.
 Mwakilishi wa MOI, Dkt. Swai akimuaga Song Tao ambaye pia amemaliza muda wake nchini.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Bw. Makwaia akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu hao na watumishi wa taasisi tatu ambazo ni  MOI, JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad