HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 June 2018

Tigo na StarTimes kukuletea Soka Moja Kwa Moja Kwenye Simu Yako ya Kiganjani, Laivu Kupitia Tigo 4G

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal. Kulia ni Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa.
Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga .
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) akikabidhiana mpira na Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.
Afisa wa Habari wa StarTimes, Sam Gisayi akionesha hatu aza kujiunga na huduma mpya ya StarTimes App itakayowezesha wapenzi wa soka kutazama mechi zote 64 za kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi. Hii ilikuwa katika katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani ambapo Tigo Tanzania na StarTimes walitangaza ushirikiano huo utakaowezesha wapenzi wa soka pia kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kujisajili kupitia Tigo namba *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa kampuni za Tigo Tanzania na Startimes wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani jijini Dar es Salaam.. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kujisajili kupitia Tigo namba *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.

Mashabiki wa soka nchi nzima wana sababu ya kushangilia kufuatia ushirikiano mkubwa kati ya Tigo Tanzania na StarTimes utakaowezesha Watanzania kutazama laivu kwenye simu zao za mkononi mechi zote za tukio kubwa zaidi la mpira wa miggu kwa mwaka 2018. Huku joto la msimu mkubwa zaidi wa soka kwa mwaka 2018 likizidi kupanda, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali ya Tigo Tanzania imetambulisha tovuti ya michezo ya www.tigosports.co.tz itakayokuwa hewani kuanzia tarehe 14 Juni mwaka huu. Tigo pia imeungana na mrushaji rasmi wa Kombe la Dunia, StarTimes kuzindua StarTimes Application, itakayowezesha wapenzi wote wa soka kuwa sehemu ya msisimko, furaha na huzuni yanayoendana na tukio hilo linalotazamwa zaidi duniani.

‘Tigo sports portal www.tigosports.co.tz itawezesha Watanzania kufurahia msisimko wa dakika zote tukio kubwa zaidi la soka duniani kupitia mtandao mpana zaidi wa Tigo 4G, pamoja na kupata habari za matukio na dondoo muhimu za tukio hilo kubwa zaidi la mpira wa miguu duniani. Kwa kujiunga kupitia huduma iliyoboreshwa ya *147*00#, wateja wetu pia wanaweza kushiriki katika shindano litakalowapa nafasi ya kushinda zawadi za hadi TSH 10 milioni,’ alisema William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo.

Tigo inajivunia kwa mara ya kwanza kabisa, kuwaletea mashabiki wa soka maajabu ya tukio hili kubwa zaidi la soka moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi. Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bunifu zinazoboresha maisha yao ya kidigitali.

Kwa kupakua StarTimes Application inayopatikana kupitia Applestore au Play Store, Watanzania sasa wanaweza kuchagua bando za saa, siku, wiki au mwezi kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#. Kisha wataweza kutazama mechi zote 64 za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 moja kwa moja kwenye simu zao janja wakiwa popote nchini huku wakifurahia ubora wa hali ya juu wa huduma za intaneti za Tigo 4G, mtandao mpana, wenye kasi ya juu na wa uhakika zaidi nchini.

‘Teknologia yetu ya StarTimes App inawezesha wateja wetu kuokoa gharama kubwa za intaneti, hivyo kuwasaidia kufurahia Kombe la Dunia muda wowote na popote walipo. Hii ni muhimu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya mechi zinaanza saa 11 jioni, muda ambapo wengi wetu bado tupo ofisini au njiani kuelekea majumbani. Kwa hiyo Startimes App na Tigo intaneti zitahakikisha kuwa hukosi mechi yoyote,’ Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa alibainisha.

‘Mtandao wetu mkubwa zaidi wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 22 nchini, pamoja na uzinduzi wa sports portal na ushirikiano huu na Startimes ambayo ni kampuni kubwa ya kidigitali nchini, tutahakikisha kuwa hakuna shabiki anayepata kisingizio cha kukosa kutazama mechi laivu, kujua matokeo na kufuatilia dondoo mbalimblai za tukio hili kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018,’ William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo alimalizia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad