HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 9, 2018

TEAM SAMATTA WAIPAPASA TEAM KIBA KWA 4-2 MBELE YA WAZIRI DKT MWAKYEMBE

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Ali Kiba  na Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva  katika mchezo wa hisani uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo , Katika mchezo huo Team Samatta imeifunga Team Kiba magoli 4-2 na kuibuka washindi wa mchezo huo mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwenye uwanja wa Taifa leo, Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na Kiwanda cha Maziwa ya ASAS DAIRIERS cha Iringa

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Mechi ya hisani baina ya marafiki wa Ali Kiba na marafiki wa Samatta imechezwa leo Jijini Dar es Salaam huku mamia ya wananchi wakijitokeza kwa wingi wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.


Mechi hiyo mahususi kwa ajili ya uchangiaji wa fedha zitakazotumika kukarabati miundo mbinu ya mashuleni iliweza kukutanisha wachezaji kutoka timu mbalimbali za ligi kuu na nje ya nchi.


Mchezo huo uliomalizika kwa Marafiki wa Samatta kuondoka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Marafiki wa Ali kiba ulikuwa ni wa ushindani kwa kila upande wakitaka ushindi.


Timu ya marafiki wa Ali Kiba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib akifunga goli la kwanza na la pili ila mpaka mapumziko timu ya marafiki wa Samatta waliweza kupata goli moja na matokeo kuwa 2-1.


Katika kipindi cha pili,Marafiki wa Samatta waliingia kwa kasi na kupata goli la pili kwa mkwaju wa penati na Haruna Moshi Boban na Mbwana Samatta kukandamiza msumari wa moto na kuleta matokeo kuwa 4-2 ila ndani ya kipindi cha pili Marafiki wa Ali Kiba walipata mkwaju wa penati ila Ali Kiba alikosa kwa kupaisha juu.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Samatta na mchezaji wa kimataifa anayecheza Genk Ubelgiji Mbwana Samatta  katika mchezo wa hisani uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo , Katika mchezo huo Team Samatta imeifunga Team Kiba magoli 4-2 na kuibuka washindi wa mchezo huo mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwenye uwanja wa Taifa leo, Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na Kiwanda cha Maziwa ya ASAS DAIRIERS cha Iringa

Mchezo huo ulikua na burudani yake hasa kwa upande wa marafiki wa Samatta kupitia kwa msemaji wa Joti ambaye aliweza kufanya mbwembwe uwanjani ikiwemo kuingia uwanjani wakati mpira ukiwa unaendelea.


Baada ya matokeo hayo,wachezaji wote wa timu mbili walionesha kufurahishwa sana na hatua hiyo kubwa waliyoifanya ya kufanikisha kuchezwa kwa mchezo huo kwa ajili ya uchangiaji wa fedha zitakazofanikisha ukarabati wa shule hususani za msingi.


Mbali na hao, wadau wengine walioweza kuhamasisha na kufanikisha mechi hiyo ni kampuni ya maziwa ya Asasi Diaries ambapo waliweza kutoa jezi kwa pande zote mbili pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa wachezaji.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Kiba na Mwanamuziki Ali Kiba kwenye mchezo wa hisani uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa kati ya timu ya mwanamuziki Ali Kiba na Mbwana Samata Mchezaji wa timu ya Genk ya Ubeligiji
Kikosi cha Team Samatta.
 Kikosi cha Team Kiba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad