HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 7, 2018

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA JINSIA NA UPATIKANAJI WA HAKI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Kwa mara ya kwanza Tanzania wanatarajia kuwa wenyeji wa mkutano wa kimataifa wa jinsia na upatikanaji wa haki utakaoshirikisha zaidi ya majaji  wakuu na wanasheria 200 kutoka katika nchi 51 za barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, Juni 7/2018,  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema  mkutano huo utakaofanyika mkoani Arusha utaanza Juni 11 hadi 13 mwaka huu.

Amesema lengo kubwa la mkutano huo ni kujadili kwa kina hali halisi ya ufuatiliaji wa haki na mazingira yanayomkumba mtu anayetaka kufikia hiyo haki.

Amesema, mkutano huo utawakutanisha watu mbalimbali wakiwemo majaji wanasheria na wadau mbali mbali wa mahakama utakuwa ni muendelezo wa majukwaa yanayofanyika sehemu mbalimbali duniani kujadiliana masuala ya haki na jinsia,

Dk. Feleshi  ameongeza kuwa, mkutano huo pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu pia utajadili na kuweka mikakati ya kuwepo kwa uwiano wa kijinsia katika mahakama zao.

Kwa upande wake, Msajili wa Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Katarina Revocati amesema Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu ndie anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo ambao wakati wa ufunguzi wanatarajia kuwa na wageni 300 hadi 400 na baada ya hapo watabakiwa na washiriki zaidi ya 200

Akizungumzia juu ya wiano wa kijinsia eneo la mahakama amesema, hadi sasa zaidi ya asilimia 45 ya maofisa wa mahakama hapa nchini ni wanawake.

“Ukiangalia hiyo asilimia utaangalia ni kwa jinsi gani mahakama zetu zinavyozingatia mambo ya jinsia bado asilimia tano tu tufikie hamsini kwa hamsini hivyo kupitia mkutano huu tutakwenda kujadili hali halisi ya ufuatiliaji wa haki na jinsia Afrika,” amesema Revocati.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Dk. Eliezer Feleshi, akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tanzania kuwa wenyeji wa mkutano wa kimataifa wa jinsia na upatikanaji  wa haki unaitarajia kuanza Juni 11 hadi 13 mkoani Arusha na kushirikisha zaidi ya majaji wakuu na wanasheria 200 kutoka katika nchi 51 za barani Afrika. Kulia kwake ni Msajili mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania, Katarina Revocati.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katarina Revokati(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa utakaojadili masuala Kijinsia,( katikati) ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi na (Kushoto) ni Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe .Dustan Ndunguru. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad