HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 12, 2018

TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA

Na Linda Shebby, Pwani 

TAASISI YA Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kasi ya kujihusisha na  vitendo  vya kupokea na kutoa rushwa  imeongezeka katika Mkoa wa Pwani.

Imeelezwa kuwa katika kipindi cha  cha Julai 2017 hadi Juni 8 mwaka huu huku Mkoa huo  umekuwa na kesi zipatazo 34 zinazoendelea  katika Mahakama mbalimbali zilizopo mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Susan Raymond ambapo ameyataja maneneo yenye kesi hizo  kuwa ni Mkuranga ,Kisarawe , Bagamoyo , Rufiji ,  Mafia , Chalinze na Ikwiriri.
Aidha Kamanda Susan amekiri kuwepo kwa changamoto katika uendeshwaji wa kesi kutoka kwa mashahidi ambao mara nyingi wamekuwa wakiharibu ushahidi pindi kesi  hizo zinapofikishwa Mahakamani.

"Hivyo kutokana na ukosefu wa uaminifu kesi nyingi zimekuwa zikipoteza ushahidi  na kushindikana kuendelea,"amesema.

Akizungumzia kuhusu kadhia hiyo amesema kuwa TAKUKURU hawatokata tamaa katika kupambana na rushwa  na kuahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa ushirikiano kwenye kesi hizo za kuzuia na kupambana na rushwa.

Amesema   kati ya kesi  34 zinazoendelea Mahakamani katika kipindi  cha Julai  mwaka 2017  hadi Juni 8 mwaka huu kesi 10 ambazo sawa na  asilimia 29.4 zinahusu  kifungu cha 15 cha sheria  ya kuzuia na kupambana na rushwa  kinachohusiana  na kosa la kushawishi, kutoa na kypokea rushwa.

Huku kesi 22 ambazo  ni sawa na asilimia 70.7 zinahusu vifungu vingine vya sheria  ya kuzuia na  kupambana na rushwa pamoja na sheria nyinginezo.

Aidha  Kamanda amesema katika kipindi hicho kesi nane zimekamilika na kutolewa hukumu  na kati ya hizo kesi sita  watuhumiwa wamekutwa na hatia  ambayo ni sawa na asilimia 75 ya kesi zote Ilizosikilizwa nankutolewa hukumu kwa kipindi tajwa.

Kamanda Susan amesema kuwa zipo hatua za kuwachukulia kisheria watu wanaoharibu ushahidi hivyo ametoa onyo na kusema  hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehusika ikiwa ni kufikishwa mahakamani mara moja.

Wakili wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Bwana Joseph Sang'wa  hapa anafafanua zaidi juu ya kifungu cha sheria ambacho kinaelezea hukumu  kwa shahidi anayepotosha ama kuharibu ushahidi wa kesi yeyote hapa aneleza zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad