HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 12 June 2018

SPRITE BBALL KINGS MSIMU WA PILI WAZINDULIWA, USAILI JUNI 16 MLIMANI CITY

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mashindano ya Mpira wa Kikapu ya Sprite BBall Kings yamezinduliwa jana usaili ukitarajiwa kufanyika Mei 16 mwezi huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall Jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa 3 asubuhi hadi sa 10 jioni.

Kituo cha East African Television (EATV), East Africa Radio kwa kushirikiana na Kinywaji cha Sprite wameanzisha mashindano hayo kwa lengo la kuinua na kurejesha heshima ya mpira wa kikapu.

Mashindano ya Sprite BBall Kings yanafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka 2017 ambapo timu ya Mchenga BBall Stars wakiondoka na ubingwa na kujinyakulia kitita cha Shiiling Milion 10 na kombe na mshindi wa pili akijinyakulia Milion 3 huku mchezaji bora wa mashindano (MVP) akipata Milion 2 na kikombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko amesema kuwa dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji katika mchezo wa mpira wa kikapu nchini.

Basilisa amesema," mashindano haya yamelenga kuinua mchezo wa mpira wa kikapu hususani kwa vijana pia kurejesha heshima ya mchezo huu unaopendwa sana na watu".

"Nawashukuru sana TBF tulikua nao mwaka jana na mwaka tunaendelea tena kuwa nao katika kuhakikisha tunarejesha heshima ya mpira wa kikapu,"amesema Basilisa.

Meneja Mauzo wa Kinywaji cha Sprite Sialouise Shayo amesema kuwa hii ni fursa nzuri ya kuinua mpira wa kikapu nchini kupitia kwa vijana walioko mtaani.

Amesema kuwa kwa muda sasa Sprite wamekuwa wanatafuta vipaji vya mpira wa kikapu katika mashule ila kwa sasa vijana wote watashiriki kuupeleka mchezo wa kikapu mbele  na lengo kuu likiwa ni kusapoti mchezo huo.

Sialouise ameongezea na kusema kupitia mashindano haya watapata wachezaji wazuri zaidi hata ikiwemo kwenda kucheza nje ya nchi

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini, Katibu Mkuu Mike Mwita amesema kuwa aanawashukuru sana EATV kwa kuanzisha mashindano haya yanayofanyika kwa mara ya pili na anaamini awamu hii yatakuwa mazuri zaidi.

Mwita ameongezea kuwa mwamko kwa mwaka huu umekuwa mkubwa sana ingawa kulikuwa na changamoto ila liliweza kutatuliwa na mashindano kuendelea huku akitoa ushauri kwa EATV na Sprite kupeleka mashindano hayo mikoani.

Katika usaili wa timu siku hiyo, atahitajika kufika nahodha wa timu husika akiwa na majina ya wachezaji wasiopungua 10, wakiwa ni raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 16 pamoja na kwenye kikosi chao wasizidi wachezaji watatu wa ligi daraja la kwanza nchini.

Mashindano hayo yatakuwa na hatua kuu sita ambazo usaili, kufuzu, kumi na sita bora, robo fainali, nusu fainali  na fainali.
Afisa Masoko wa East Africa Television ( EATV)  Basilisa Biseko (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa mpira wa kikapu nchini wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 ikiwa ni kwa mwaka wa pili yanayotarajiwa kuanza mwishoni kwa mwezi June, kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Mike Mwita na Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji ya Sprite Sialouise Shayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad