HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 June 2018

RAIS DK.SHEIN AWAFUTARISHA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemedi Suleiman (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Mhe.Rashid hadid Rashid mara baada ya Swala ya Magharibi jana kabla ya Futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini  Pemba jana katika Futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar kabi
 Baadhi ya  Mashekhe wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pembaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
 Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake,Wilaya ya Chakechake ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akijumuika na Viongozi akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.
 Baadhi ya  akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman akitoa Shukurani kwa Niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kwa ushiriki wa Wananchi wa Mkoa huo katika Futari  aliyoiandaa jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya  Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad