HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 13, 2018

MKURUGENZI MKUU TCAA ATHIBITISHWA KUWA MWENYEKITI WA CANSO KANDA YA AFRIKA

Shirikisho  la Kimataifa  la Huduma za Anga na uongozaji Ndege, maarufu kama (CANSO), katika mkutano wake mkuu wa 22 wa mwaka uliofanyika tarehe 12/06/2018 huko Bangkok, Thailand, limemthibitisha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari, kuwa Mwenyekiti mpya wa CANSO kanda ya Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Hii inafuatia uteuzi wa Bwana Johari kuwa Mwenyekiti wa CANSO Afrika Machi 2018 huko Madrid, Hispania. Kwa wadhifa huo Bwana Johari anakuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji (EXCOM) ya shirikisho hilo muhimu la kimataifa katika usafiri wa anga.
Bi Terri Bristol, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Marekani anaendelea kuwa Mwenyekiti wa CANSO  ambapo, Bwana Rudy Keller kutoka Canada ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti
Wajumbe wengine wa EXCOM ni Martin Rolfe -Uingereza,Klaus Dieter Scheurle -Ujerumani,  Hamza S. Johari - Tanzania, Mark Cooper- Uingereza, Augustin Rodrigues Grellet - Agentina, Jan Klas - Jamhuri ya Czech, Don Thoma - Marekani, Dr Saleh Al Ghamdi - Saudi Arabia, Kevin Shum - Singapore and Captain Gilbert Kibe - Kenya.
Wajumbe wa EXCOM wanakutana mara nne kwa mwaka kupanga mikakati ya uongozaji safari za ndege na masuala mengine ya kisera kuhakikisha usalama na ufanisi wa usafiri wa anga duniani.
Menejimenti ya Shirikisho la CANSO inaongozwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wake Mkuu Jeff Poole akishirikiana na wafanyakazi wengine wa sekretariati ambayo inahakikisha utekelezaji wa maagizo na mikakati ya kamati kuu ya EXCOM
Tunamtakia Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari Heri na Mafanikio katika majukumu yake mapya katika jumuiya hii ya kimataifa.
Imetolewa  na Kitengo cha Habari -TCAA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad