HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 June 2018

Mfumuko wa bei wapungua hadi kufikia asilimia 3.6

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MFUMUKO  wa bei wa Taifa  wa Mei 2018  umepungua  hadi kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na asilimia 3.8 ilivyokuwa Mwezi Aprili 2018 mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa bei kumechangiwa sana na kupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula.

Amesema  baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mahindi kwa asilimia 10.3, unga wa mahindi kwa asilimia 12.5, mtama kwa asilimia 13.8, unga wa mihogo kwa asilimia 15.2, viazi mviringo kwa asilimia 9.0 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.6, alisema bwana Kwesigabo.

Ameongeza kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2018.

Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 nchini Uganda umepungua hadi asilimia 1.7 kutoka asilimia 1.8 kwa mwaka ulioishia mwezi aprili 2018.

Aidha kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.95 kutoka asilimia 3.73 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2018.

Mfumuko wa bei unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mfumko wa bei wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Mfumuko wa bei umeshuka toka asilimia 3.8 mwezi Aprili hadi kufikia 3.6 Mei. Kushoto ni Meneja wa Ajira na Bei toka NBS, Ruth Minja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad