HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 June 2018

Klabu ya kuogelea ya Bluefins kuishiriki mashindano ya Kenya

Jumla ya waogeleaji 11 wa klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins watashiriki mashindano ya Mombasa yaliyopangwa kuanza leo.

Mashindano hayo ya kimataifa, yanashirikisha waogeleaji mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki na klabu hiyo ndiyo pekee inayoiwakilisha nchi.

Muasisi na kocha mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja wachezaji ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano hayo kuwa ni Aminaz Kachra, Lina Goyayi, Muskan Gaikwad na Aliyana Kachra ambao ni wanawake.

Waogeleaji wa kiume ni Delbert Ipilinga, Christian Fernandes, Parth Motichand, Isaac  Mukani, Sahal Harunani, Aaron Akwenda na Hassan Harunani.
Alisema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo pamoja na kushiriki kwa mara ya kwanza katika historia.

“Haya ni mashindano yetu ya kwanza ya nje ya nchi tokea klabu yetu ianzishwe, na tumeamua kufanya hivi baada ya kupata mafanikio makubwa sana katika michezo ya ndani kwa kushika nafasi ya pili na ya tatu, tumeona kuwa ni wakati sasa kwa waogeleaji wetu kuvuka mipaka ya nchi na kupima uwezo wao,” alisema Alidina.

Alifafanua kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo ili kuiletea sifa Tanzania.
“Napenda kuishukuru BMT na Kamati ya Muda ya chama cha kuogelea nchini kwa kutupa msaada mkubwa pamoja na vibali, tumefarijika sana na tunahidi kuleta ushindi katika mashindano hayo,” alisema Alidina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad