HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 27 June 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA AWATAKA WAAJIRI KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NCHINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAAJIRI nchini watakiwa kutumia fursa ya uboreshwaji ya mazingira kazi ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje hususani kwenye viwanda  kwani Serikali ya awamu ya tano imejizatiti kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua kupitia viwanda.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Ole Sante Gabriel wakati wa mkutano wa mwaka  wa 59 wa chama cha waajiri nchini uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Mkutano huo wa mwaka huu ukiwa ni wa 59 uliolenga katika mageuzi ya udhibiti ili kuboresha mazingira ya biashara  ikiwemo katika kudhibiti na kupitia sera ya serikali ya awamu ya tano imeweka mkakati wa kuboresha mazingira ya biashara ambayo yatavutia wawekezaji wa ndani na nje.

Ole Sante amefungua mkutano huo uliohudhuriwa na wadau kutoka sekta tofauti alisema ili uchumi ukue unabidi kuwe na mafiga matatu, waajiri, wafanyakazi na serikali kwa pamoja wanashirikiana kukuza uchumi.

"Katika bajeti ya mwaka 2018/19  Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango amezitaja changamoto  zinazokwamisha uwekezaji na mazingira ya kibiashara ikiwemo sheria na kanuni za uanzishaji wa biashara, gharama kubwa za kodinna ada," amesema Prof Ole Sante Gabriel.

Mkurugenzi  Mtendaji wa ATE Dr Aggrey Mlinuka amesema kuwa kila mwaka wamekuwa wanafanya mkutano huu wa wanachama na mwaka huu wameangalia zaidi mageuzi ya kibiashara ili kuweza kuyaboresha kwa kusaidana na serikali ili kuvutia zaidi wawekezaji.

Dr Mlinuka amesema kuwa umedhamiria kuboresha mazingira mazuri kwa wafanyakazi ikiwemo mifuko ya jamii ya wafanyakazi na sekta ya afya.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof Ole Sante Gabriel akizungumza na waajiri kutoka sekta mbalimbali Nchini wakati wa mkutano wa 59 wa mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Jijini Dar es salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Jayne Nyimbo akizungumza  na waajiri kutoka sekta mbalimbali Nchini wakati wa mkutano wa 59 wa mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Nchini (TUCTA)  Dr Yahya Msigwa akizungumza na wadau kutoka sekta mbalimbali za waajiri na kuelezea changamoto wanazokabiliwa nazo wafanyakazi kwenye mkutano uliofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dr Aggrey Mlinuka akizungumza na waandishibwa habari kuhusiana na mkutano wa 59 wa mwaka wa Chama cha Waajiri ukiwa na madhumuni ya mageuzi katika kuboresha utendaji kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezekaji Prof Ole Sante Gabriel akiwa katika Picha ya pamoja na wadau wa sekta ya waajiri nchini.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad