HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 June 2018

KAMPUNI YA SIHEBS TECHNOLOGIES YAZINDUA HUDUMA MPYA YA NITUME

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
KAMPUNI ya kutoa huduma ya mfumo ya Tehama, ya Sihebs Technologies, imezindua huduma mpya ya teknolojia ijulikanayo kwa jina la Nitume itakayowawezesha wananchi kuagiza bidhaa mbalimbali kwa kutumia simu zao za mkononi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa App hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa Sihebs Siwangu Mgata amesema App hiyo ya Nitume inaweza kupakuliwa bila ya malipo ya zaida na watumiaji wa simu za mkononi wanaotumia mfumo wa iOS na Android imetengenezwa ili kuendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya simu za mkononi na mfomu wa Tehama.

"App hii ya Nitume inamuwezesha mtumiaji wa simu ya mkononi popote alipo nchini kuagiza bidhaa kama vile chakula, dawa, vitu vya nyumbani na bidhaa zingine mbali mbali kutoka kwa muuzaji wa bidhaa umpendae na Nitume itakuletea mpaka mahali ulipo," amesema Mgata.

Amesema App hiyo pia itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo kutafuta wauzaji wa bidhaa waliokaribu nao kupitia simu zao za mkononi na kusoma  maoni ya watumiaji wengine kuhusu ubora wa budhaa na huduma ili kujipatia bidhaa bora.
Amezitaja huduma zingine zipatikanazo kwenye App hiyo ni Nitume biashara itakayowawezesha wafanyabiashara kufikiwa na wateja wengi huku nitume fikisha ikiwawezesha wasafirishaji kufikisha bidhaa za wateja kwa uaminifu mkubwa.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutoa huduma ya mfumo ya Tehama, ya Sihebs Technologies Siwangu Mgata akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa  huduma mpya ya teknolojia ijulikanayo kama Nitume itakayowawezesha wananchi kuagiza bidhaa mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi. Kulia kwake ni Meneja Mradi Rodrick Ngowi na kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Deborah Masaru
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutoa huduma ya mfumo ya Tehama, ya Sihebs Technologies Siwangu Mgata akiwaonyesha waandishi wa Habari hawapo pichani jinsi ya kufungua App ya Nitume itakayowawezesha wananchi kuagiza bidhaa mbalimbali kwa kutumia simu zao za mkononi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad