HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 18 June 2018

KAMPUNI YA EY YAWAKUTANISHA WADAU KUCHAMBUA BAJETI 2018/ 19

 KAMPUNI ya EY imewakutanisha wadau wakiwamo wachambuzi wa bajeti ambapo pamoja na kuipongeza bajeti ya fedha ya mwaka 2018/2019 wameishauri Serikali kuwekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza viwanda na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Wakizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kujadili bejeti ya Serikali iliyowasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango wadau hao kila mmoja aliyepata nafasi ya kutoa maoni yake wameipongeza lakini wakatoa ushauri kwa baadhi ya maeneo ambayo wanaamini yakitiliwa mkazo italeta tija katika maendeleo ya nchi.

Miongoni mwa waliochangia na kuichambua bajeti ya mwaka huu ni Mtalaam na Mchambuzi wa bajeti Profesa Prosper Ngowi ambaye amesema Serikali inatakiwa kuwekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo ambayo itaongeza ukuaji wa viwanda na kuchochea ajira kwa wananchi.

Amefafanua katika sekta ya kilimo, Serikali ya Tanzania imeridhia makubaliano yaliyoingiwa na nchi mbalimbali za kuongeza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 lakini ukifuatilia utabaini kilimo kinakuwa kati ya asilimia 3 hadi asilimia 5.
 Mtalaam na Mchambuzi wa bajeti Profesa Prosper Ngowi akizungumza jambo wakati wa kujadili bejeti ya Serikali, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam leo.

"Bajeti ya Serikali ya mwaka huu ni nzuri na unapotaka kuchambua bajeti lazima uangalie na bajeti za mwaka uliopita.

"Unapoangalia bajeti imekuwa na maendeleo kila mwaka lakini kikubwa ambacho tunataka kuona ni utekelezaji wa bejeti yenyewe,"amesema Profesa Ngowi.
 Hata hivyo bajeti kwa ujumla iko vizuri na kufafanua ni wakati muafaka pia kwa Serikali kuhakikisha inatoa fursa zaidi katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati ambao wakijengewa uwezo kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza wigo wa ajira

Mtoa mada na mchambuzi mwingine kwenye mjadala huo Felix Mlaki amesema kuwa kuna baadhi ya mambo lazima yaangaliwe vizuri ambapo amesema kwa upande wake hakubaliani na kutengwa fedha kwa ajili ya kutoa kwa wananchi.

"Kuna utaratibu ambao unafanyika wa kutengwa fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana.Kwangu sioni kama hili linatija na ushauri wangu badala ya kutoa fedha.
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mokasi Medical Systems, Monica Joseph akizungumza jambo wakati wa kujadili bejeti ya Serikali, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam leo.

"Ni vema Serikali ikatengeneza mazingira ya kuwadhamini wananchi katika kuanzisha miradi ya kimaendeleo.Pia lazima watu walipe kodi kikamilifu,"amesema Mlaki.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mkazi wa Ernest &Young Joseph Sheffu amesema lengo la kuandaa mjadala huo wa kuichambua bajeti ni kupata maoni ya wateja wao hasa kwa kuzingatia bajeti husaidia wafanyabiashara kupanga mikakati yao na kuangalia namna ya kuitekeleza.

Sheffu amesema bajeti iliyowalishwa na Waziri wa Fedha kwa mwaka huu ni nzuri."Tunaamini mjadala huu wa kuichambua bejeti unatoa fursa kwa wafanyabiashara kuweka malengo yao ya kibiashara,"amesisitiza Sheffu.

Mtoa mada mwingine kwenye mjadala huo Monica Joseph ameipongeza bajeti ya mwaka huu kutokana na namna ambavyo imejikita katika kuimarisha sekta ya kilimo, kusaidia wajasiriamali pamona na makundi mbalimbali yakiwamo ya wanawake na vijana.
Sehemu ya Wadau waliohudhulia majadiliano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad