HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 13 June 2018

HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA MAMC, MLOGANZILA WAADHIMISHA SIKU YA KUCHANGIA DAMU

Mtaalamu kutoka kitengo cha kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) akielezea faida za kuchangia damu na sifa za mtu anayetakiwa kuchangia damu kwa wafanyakazi ya Benki ya Mkombozi waliojitolea kuchangia damu katika kuadhimisha siku ya kuchangia damu duniani.
Wataalamu kutoka kitengo cha cha kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) wakiwa wanapima vipimo mbalimbali kwa wachangiaji kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Bw. George R. Shumbusho (kulia) akishiriki katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wakisubiri kuchangia damu katika kuadhimbisha siku ya kuchangia damu duniani
Kwa Niaba ya Mkurugenzi mtendaji Bw.Antony Mnyambo akimkabidhi kitanda na mabox 20 (cooler boxes) kwa Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) Dkt. Ivan Nyamhanga kwa ajili ya kusaidia zoezi la uchangishaji damu.
Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) Dkt. Ivan Nyamhanga akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkombozi Benki baada ya kupokea vifaa vya kutumika wakati wa zoezi la uchangishaji damu.
Picha ya Pamoja ya wataalamu kutoka Kitengo cha Kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) wakati wa maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani.

Na Mwandishi Wetu.
Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili MAMC, Mloganzila imeanza maadhimisho ya siku ya kuchangia damu kwa kufanya zoezi la uchangishaji damu kwa wafanyakazi wa Mkombozi Commercial Bank, tawi la Msimbazi Center ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wanaohitaji.

Katika zoezi hili la uchangizaji damu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mkombozi Bw.George R. Shumbusho alitoa msaada wa kitanda kimoja kwa hospitali ya MAMC kwa ajili ya kusaidia wakati wa zoezi la utoaji damu kwa watu mbalimbali wanaojitolea na mabox 20 (cooler boxes) za kuhifadhia damu wakati wa kupeleka damu wodini kwa wagonjwa. Msaada huu wa vifaa unagharimu pesa ya kitanzania shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000)

Akiongea wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Shumbusho “Kama taasisi ya benki kwa kuona umuhimu wa mahitaji ya damu ndiyo maana tumeadhimisha siku hii ya leo kwa kuwaamasisha wafanyakazi wetu wachangie damu ili tuweze kuokoa maisha ya watanzania na kutoa msaada ya vifaa vitakavyoweza kusaidia zoezi la uchangishaji damu”, alisema

Vile Vile aliwapongeza wafanyakazi waliojitokeza kuchangia damu, “Ni jambo la umuhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa”, aliongeza.

Naye Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba MAMC, Mloganzila Dkt. Ivan Nyamhanga amewashukuru uongozi mzima wa Benki ya Mkombozi kwa kuhamasisha zoezi hili la kuchangia damu na pia kwa vifaa walivyotoa ambavyo vitasaidia wakati wa zoezi la uchangishaji damu.

Pia aliwashukuru wafanyakazi wote wa benki ya Mkombozi kwa kujitolea kuchangia damu kwa wahitaji. "Kama mnavyojua mahitaji ya damu ni makubwa hasa katika hospitali yetu ambayo bado ni changa na hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kuhamasika kuchangia damu", alisema Dkt. Nyamhanga.

Zoezi hili la maadhimisho ya siku ya kuchangia damu lilifanyika katika Benki ya Mkombozi, tawi la Msimbazi center na vile vile baadhi ya maaskari kutoka SUMA JKT, Mloganzila waliweza kuchangia damu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad