HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 June 2018

EXIM BANK TANZANIA LIMITED KUTUNISHA MFUKO WA MIKOPO KWA SME HAPA NCHINI

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu akipeana mkono na Marleen Jansen, Afisa Mkuu wa Uwekezaji, wa benki ya Maendeleo ya Uholanzi – FMO baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa shilingi bilioni 75 ili kuwekeza kwenye mfuko wa mikopo ya muda mrefu wa biashara ndogo ndogo na za kati (SME) nchini Tanzania.

BENKI ya Exim Tanzania imetangaza kuchukua mkopo wa kiasi cha shilingi bilioni 75 kutoka kwa benki ya Maendeleo ya Uholanzi – FMO, ili kuwekeza kwenye mfuko wa mikopo ya muda mrefu wa biashara ndogo ndogo na za kati (SME) hapa nchini 

Benki imechukua mkopo huo ili kuziba pengo kubwa la mikopo kwa biashara ndogo ndogo na za kati nchini ambazo zinakadiriwa kuwa ni takribani kampuni milioni 3. Vilevile utafiti unaonyesha kuwa idadi kubwa ya kampuni hizi (zinazoajiri watu chini ya watano) zinamilikiwa na familia na zinapatikana hasa katika miji midogo na maeneo ya vijijini.

Ingawa takwimu za kiutafiti kwenye biashara ndogondogo na za kati sio za kutosha, data zilizopo zinaashiria kuwa SME ni sekta yenye umuhimu mkubwa katika uchuni. Kampuni hizi nyingi huwa hazina nafasi ya kupata huduma za kifedha ingawa kuna asilimia ndogo ambayo inategemea huduma za kifedha kutoka kwenye taasisi zisizo za kifedha kama vile kupitia mitandao ya simu ambapo huduma za kutuma fedha ni gharama kubwa. 

Akizungumzia hatua hiyo ya benki ya Exim, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Jaffari Matundu alisema "Hatua hii ni samabamba na dira ya Mheshimiwa, Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ya kutaka kubadilisha Tanzania kuwa ya nchi inayotegemea uchumi wa viwanda.

 Sekta ya SME inachukuliwa kuwa injini muhimu katika kuleta ukuaji katika uchumi wowote na uchumi wowote wa kutegemea viwanda na ni lazima kuwe na idadi kubwa ya SME ili kusapoti makampuni na miradi mikubwa. Miradi mikubwa katika sekta ya miundombinu itahitaji huduma mbali mbali kwa ajili ya kuhakikisha kukamilika kwa miradi hii. Mkopo huu usio na dhamana wa shilingi bilioni 75 kutoka benki ya Uholanzi -FMO ni sehemu ya mkakati wa benki yetu ili kusaidia sekta ya SME kuongeza ajira na kupunguza umaskini nchini. "

"FMO tuko radhi kuendelea na kuimarisha uhusiano wetu na Benki ya Exim kupitia mkopo huu. Kusaidia makampuni ya ndani kupitia washirika wa kuaminika kama Benki ya Exim ni msingi wa ujumbe wa FMO, "Marleen Jansen, Afisa Mkuu wa Uwekezaji, FMO.

Mkopo huu ni ushuhuda tosha wa imani na sifa nzuri ambayo taasisi za maendeleo za kifedha duniani zimewekea benki ya Exim. Benki ya Exim ina uhusiano na mashuhuri wote DFIs viz. IFC, EIB, PROPARCO na zaidi mkopo wa pili na FMO imekuwa heshima kubwa. Benki ya Exim itatoa kwa mara moja shilingi 23 bilioni na zilizobaki kwenye kipindi cha miezi 17 ijayo.

Benki ya Exim ni Benki ya kwanza Tanzania kuweka alama nje ya nchi na kwenda kimataifa na sasa iko katika nchi 3 Kisiwa cha Comoro, Djibouti na Uganda. Benki ya Exim imepatiwa tuzo ya “Benki bora ya mwaka 2017 kwa wateja binafsi na biashara ndogo ndogo katika tuzo za mabenki za Afrika mashariki iliyotolewa Mei'17 na Muajiri Bora katika Utawala wa Rasilimali Watu na Ushirikishaji wa wafanyakazi kwa mwaka wa 2016 na Chama cha Waajiri Tanzania. Jumla ya Mfuko wa Mali na hisa kama ilivyo tarehe 31 Desemba 2017 ni TZS 1.6 Trillion na TZS 231 Bilioni kwa mtiririko huo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad