HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 9 June 2018

DCB WAJITOSA UDHAMINI NDONDO CUP, YAAHIDI KUTOA ELIMU YA HUDUMA ZA KIBENKI

Meneja Masoko wa Benki ya DCB Boyd Mwaisame akielezea namba watakavyokuwa wanawafungulia akaunti wachezaji na timu shiriki kupitia zawadi wakatazokuwa wanazitoa.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uzinduzi wa Michuano ya Ndondo Cup iliweza kufunguliwa rasmi jana kwa timu ya Mabibo Market kuchuana na Keko Furniture uliofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa kwanza Mabibo Market waliweza kuondoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Keko ukiwa ni katika hatua ya makundi ya 32 bora.

Kwenye michuano ya mwaka huu, Benki ya DCB imeweza kudhamini kwa mwaka huu na kuahidi kutoa hela za washindi wa kila mchezo sambamba na mchezaji bora wa mechi.

Akuzungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Meneja Masoko wa DCB Boyd  Mwaisame amesema kuwa kwa mwaka huu wameamua kuja kudhamini michuano hiyo ya Ndondo Cup ikiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa wachezaji na timu kuweza kufungua akaunti za benki ili kuhifadhi fedha zao kwa usalama zaidi.

Boyd amesema kuwa katika zawadi wakatazokuwa wanatoa kwa timu itakayokuwa inashinda kwenye michuano ambapo ni sawa na kiasi cha shillingi laki mbili (200,000) moja kwa moja fedha hizo zitafunguliwa akaunti ya timu sambamba na mchezaji bora wa mechi yeye fedha yake atafunguliwa akaunti binafsi.

"Sisi kama DCB tumeonelea sana kuwa timu zote pamoja na wachezaj kuwa na akaunti za benki maana hata fedha za ushindi  watakazokuwa wanazipata ziwe zinapitia kwenye akaunti kitu ambacho kitakuwa ni kizuri zaidi, na kwa kuanzia leo tunaanza timu ya Mabibo Market iliyoshinda pamoja na mchezaji bora wa mechi wote kwa pamoja watafunguliwa akaunti zao hapa hapa,"amesema Boyd.

Pia, Boyd ameema kuwa pamoja na udhamini huo wanataka kutoa elimu ya huduma za kibenki kwa vijana wengi na timu zinazoshiriki mashindano hayo ya Ndondo Cup ili wazitumie na kuwanufaisha kiuchumi huku wakiwa na lengo la kusaidia kuendeleza mpira wa soka nchini.
Msanii Nikki Wa Pili akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup iliyozinduliwa jana katika Uwanja wa Kinesi Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Masoko wa benko ya DCB Boyd Mwaisame.

Mbali na hilo DCB waliweza kumtambulisha Balozi wao msanii Nikki wa Pili  ambaye aliweza kuwashauri vijana hususani wachezaji kuweza kufungua akaunti ya benki ambapo wanaweza kupata hadi mikopo pindi pale wanapokwama.

Uzinduzi huo uliweza kuhudhuriwa na wachezaji mbalimbali akiwemo mchezaji wa Kimataifa wa Kenya Victor Wanyama  anayekipiga ligi ya Uingereza katika timu ya Tottenham Spurs, Mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta, Mrisho Ngasa na wachezaji wengine mbalimbali.
Wachezaji wa Kimataifa Victor Wanyama na Mbwana Samatta wakiwa wanafuatilia mtanange wa uzinduzi baina Ya Mabibo Market na Keko Furniture.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Wallace Karia akimkabidhi fedha kiasi cha Shilling Elfu Hamisini (50,000) mchezaji bora wa mechi kutoka timu ya Mabibo Market Nassor Kapama baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Aidha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Wallace Karia aliweza kutoa neno kwa waandaji wa michuano hiyo kuendelea kuibia vipaji vya wachezaji wachanga kwani wengi wao wanatokea katika timu za kawaida.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad