HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 14 June 2018

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), ambayo pia ni mtandao wa radio zenye maudhui ya kijamii nchini. Mtandao huu una radio 31 wanachama zilizopo Tanzania bara na visiwani.
 Chini ya mkataba huo, OUT itatumia wataalam wake (wahadhiri) kushiriki katika vipindi mbalimbali vyenye manufaa kwa umma wa watanzania hususan wananchi wanaoishi vijijni, ambapo radio jamii zinafanya shughuli zake. Pia TADIO kupitia radio wanachama, itawajibika kurusha vipindi hivyo kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya. 
Mkataba huo unaipa fursa TADIO kuwa na ofisi zake katika majengo ya Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria, Kinondoni Dar es Salaam. Pia unatoa fursa kwa wanafunzi wa OUT wa taaluma ya habari na mawasiliano, kutumia studio zilizopo katika majengo hayo zinazomilikiwa na TADIO kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
 Pamoja na kutumia studio hiyo, wanafunzi wa OUT watapata pia nafasi ya kushiriki mafunzo kwa vitendo katika radio wananchama zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda akitoa rai juu ya mkataba huo amesema “OUT itatumia mtandao wa radio wanachama wa TADIO kuifikia jamii na kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali za kiuchumi na maendeleo zilizopo kwa kuzingatia vigezo vya utafiti. 
Wataalam waliopo chuoni wakitumika vyema, adhima ya kujenga Tanzania yenye viwanda itafikiwa mapema. 
Lakini pia OUT itashirikiana na TADIO kuendesha semina, mikutano, na makongamano mbalimbali kuhusu masuala yenye tija kwa jamii. OUT inaitumia TADIO kwakuwa inawapa fursa ya kuwafikia walengwa wao waliopo hadi vijijini. 
Pia katika kuwainua kielimu wanahabari, OUT itatoa fursa kwa wafanyakazi na wanachama wa TADIO kudahiliwa na chuo hicho kupitia matawi yake popote nchini chini ya utaratibu wa kuchangia gharama”.
Mwenyekiti wa TADIO Ndugu Prosper Kwigize amesema “Fursa ya kuchangia gharama za masomo iliyotolewa, iwe chachu kwa waandishi na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini kujiendeleza kielimu. Amezitaka pia radio jamii kutoa ushirikiano kwa watumishi wa OUT popote walipo nchini kwa manufaa ya umma wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha UNESCO Bi. Nancy Kaizilege, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda pamoja na Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Mwenyekiti wa TADIO Ndg Prosper Kwigize na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha UNESCO Bi. Nancy Kaizilege wakisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano baina ya TADIO na OUT iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria (OUT) na TADIO wakati wa hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda wakionyesha hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria (OUT) na TADIO mara baada ya kusainiwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, UNESCO na OUT baada ya hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya OUT na TADIO. Kutoka kushoto walioketi ni Bi. Nancy Kaizilege (UNESCO), Prof Elifas Bisanda (VC OUT), Prosper Kwigize (Mwenyekiti TADIO) na Marco Mipawa (Katibu TADIO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad