HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 21 June 2018

BODI YA PSPTB: SOMO LA HESABU LATAJWA KUWA CHANGAMOTO

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
BODI ya wataalumu wa Manunuzi  na Ugavi (PSPTB)nchini imesema ni vema somo la hisabati likatiliwa mkazo kuanzia shule ya msingi  ili kuwezesha kupatikana kwa wahitimu wanaostahili kukabidhiwa ofisiM

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya PSPTB,  Godfred Mbanyi amesema hayo leo jijini  Dar es Salaam na wakati wa kutangaza matokeo ya 16 ya mitihani ya bodi hiyo.

Amesema licha ya jitihada zote ambazo zimekuwa zikichukuliwa na bodi hiyo kuhakikisha kuwa wahitimu wa fani hiyo wanafanya vizuri kwenye somo la hesabu lakini bado ufaulu umeendele kuwa hafifu jambo ambalo linaleta shaka kwa wataalamu hao kukabidhiwa ofisi.

Amesema ingawa katika matokeo haya ya 16 ya mitihani ya bodi ufaulu umeongezeka kwa asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka jana, lakini bado kuna ufaulu hafifu kwenye masomo yanayohusisha hesabu.

“ Somo la hesabu bado ni changamoto kubwa katika Jamii, wahitimu wengi wamekuwa hawana msingi mzuri wa somo la hesabuheh wakiwa chini, jambo ambalo linaongeza changamoto, ni vigumu kwa muhitimu wa aina hii kumkabidhi Ofisi kutokana na kushindwa kumudu sawasawa mahesabu,

Amesema kuwa pamoja na matokeo hayo kama bodi wataendelea kubuni mbinu nyingine ambazo zitasaidia kurahisisha ufaulu kwenye somo hilo.

Mbanyi amevitaja vyuo vilivyofanya vizuri kwenye mitihani hiyo kuwa ni Chuo cha Ushirika Moshi, Chuo cha Biashara CBE na Chuo cha Mtakatifu Augustine cha Mwanza katika ngazi ya nne.

 Aidha amesema, bodi imeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wahitimu ili waweze kufanya vema katika mitihani yao, "mtu yeyote anayetaka kuja kufanya mitihani ya bodi ni vema awe tayari kuhudhuria mafunzo ya kujitayarisha ili kuongeza idadi ya watahiniwa wanaofaulu" amesema Mbanyi.

“Kwa sasa tunaweka mikakati ya kuboresha ufundishaji ili kuweza kuongeza ufaulu kwa wahitimu kwani licha ya kuongezeka ufaulu kwa asilimia 11 matokeo bado siyo mazuri sana, hata hivyo ni lazima kuwe na mkakati bora Zaidi wa kutilia mkazo somo hili kuanzia chini,” amesema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa bodi hiyo, Amani Ngonyani amesema  bodi itahakikisha inaendelea kufanya ziara za mafunzo katika vyuo vinavyotoa taaluma hiyo nchini ili kuwakumbusha wanafunzi juu ya kutilia mkazo taaluma hiyo.

“Tutatembela vituo vyote nchini ili kuona kama vina sifa na uwezo w akufundisha ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo kwa ajili ya kupika na kutoa wanafunzi wenye sifa na uwezo unaohitajika katika taaluma hii,” amesema.

Pamoja na kutunukiwa cheti cha Bodi, wahitimu 809 kati ya 1549 waliofanya mitihani hiyo Mei Mwaka huu ikihusisha vituo tisa wahitimu hao pia wanatarajiwa kutunukiwa vyeti vya kimataifa kwenya maafali itakayofanyika Oktoba mwaka huu, 
 Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi  na Ugavi, PSPTB akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kutangaza matokeo ya 16 ya mitihani ya bodi hiyo. Iliyofanyika Mei mwaka huu ambayo mahafali yake yatafanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa bodi hiyo, Amani Ngonyani
Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa bodi  ya wataalumu wa Manunuzi  na Ugavi, PSPTB , Amani Ngonyani akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari juu ya mikakati inayowekwa na bodi hiyo ya kuboresha ufundishaji ili kuweza kuongeza ufaulu kwa wahitimu wakati wa utangazwaji wa matokeo ya 16 ya mitihani ya bodi hiyo. Iliyofanyika Mei mwaka huu ambayo mahafali yake yatafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad