HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 23 June 2018

BENKI YA NBC YAZINDUA MTANDAO WA NBC WAKALA KWA WATEJA WAO

Na Agness Francis, Globu ya jamii
BENKI ya NBC  imezindua ramsi mtandao wa NBC Wakala kwa wateja wao wote  na  wale wasiotumia huduma ya benki  hiyo.

NBC Wakala ni fursa  inayolenga kutoa huduma za kibenki nje ya mtandao wa matawi na mashine za kutolea fedha za ATM kwa mawakala wenye mikataba.

Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa benki NBC Theobald Sabi amesema benki hiyo imedhamiria kutoa huduma za kibenki kwa Watanzania na wateja wao  kuwataka kufika kwenye matawi hayo.

"Kwa Kupitia NBC Wakala wateja wetu wataweza kupata huduma za kibenki katika maeneo ambayo yako karibu zaidi kwao Kupitia mtandao wa matawi 50 na ATM zaidi ya 2000 zilizosambaa nchi nzima,  lakini kupitia NBC Wakala benki yetu inazidi kuwa karibu na wateja wake," amesema Sabi.

Sabi amesema kuwa Uzinduzi wa NBC Wakala ni moja ya mpango mkakati wa kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wateja kwa njia rafiki na kwa ukaribu zaidi ambayo ni kati ya mifumo yetu ya ugavi tunayoiwekea mkazo kwa maana inapanua wigo na mtandao wa utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Aidha Sabi amesema kuwa huduma hiyo ya  NBC Wakala ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali wanaotaka kushiriki katika biashara ya utoaji huduma za kibenki,ambapo pia ametoa mwito kwa wajasiriamali wanaohitaji kushiriki katika fursa hiyo wajitokeze bila kuhofia.

Mkurugenzi huyo  ameongezea kuwa ili kuwa Wakala wa NBC, mjasiriamali atatakiwa kuwa na leseni ya biashara, sehemu ya biashara ya kudumu na awe anaendesha biashara ya kwa muda usiopungua miaka miwili.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi kulia na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Filbert Mponzi wakionyesha bango baada ya kuzindua huduma ya NBC Wakala jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa huduma za NBC Wakala Jacqueline Sindano (kulia) akimkabidhi  mmoja wa wakala wa NBC Wakala Humud Ali Salum mashine maalum ya POS baada ya uzinduzi wa NBC Wakala  jijini Dar es Salaam, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi
Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki ya NBC Filbert Mponzi (kulia) akimueleza mmoja wa wakala wa NBC Humud Ali Salum(kushoto) jinsi ya kutumia mashine maalum za POS wakati wa kuzindua huduma na NBC Wakala leo jijini Dar es Salaam, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad