HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 28, 2018

Bei ya Ufuta katika wilaya ya Kibiti yazidi kupaa

*Ni kutokana na mfumo wa stakabadhi ghalani

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BEI ya ufuta katika wilaya ya Kibiti imezidi kupaa kutoka shilingi 2750 hadi 3100 kwa kilo na kufanya wakulima kunufaika na kilimo hicho.

Kupanda kwa bei hiyo kunatokana na serikali kutaka mazao ya korosho, pamba pamoja na ufuta kuuzwa kwa mfumo wa mnada wa stakabadhi ghalani ikiwa ni kumsaidia mkulima kunufaika na kilimo anachokifanya.

Akizungumza wakati wa mnada wa zao la Ufuta Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti  ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Milongo Sanga amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa mnada zao la Ufuta limekuwa na soko kubwa na kufanya wananchi kunufaika kilimo hicho.

Amesema kuwa baadhi ya wachuuzi walikuwa wakinunua zao la Ufuta kwa shilingi 1200 hali ambayo kuliwafanya baadhi wakulima kuachana na kilimo lakini mfumo wa mnada kutokana na maagizo ya serikali wakulima wameanza kunufaika na mfumo huo.

Sanga amesema kuwa wananchi waachane na wachuuzi wa zao la ufuta kwani hawana nia njema na wao katika kuwakomboa kiuchumi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti, Alvera Ndabagoye amesema kuwa tangu kuanza kwa mnada huo bei imekuwa ikipanda kila mnada unapofanyika pamoja na tani za ufuta zikiongezeka.

Amesema mnada wa kwanza waliuza ufuta  wa Tani 90 kwa shilingi 2750, Mnada wa pili waliuza ufuta wa Tani 118 kwa shilingi 2781 huku mnada wa tatu wameuza ufuta wa tani 454.8 kwa shilingi 3100.

Amesema kuwa anategemea mnada wa Julai 4 mwaka huu bei inaweza kupanda huku akisisitiza wanunuzi wanaoshinda mnada kulipa kwa wakati ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wakulima.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti , Milongo Sanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mnada wa zao la Ufuta uliofanyika katika viwanja makao makuu ya wilaya hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Khatib Chaulembo akizungumza kuhusiana wanunuzi wa ufuta kulipa malipo kwa wakati kabla ya kuingia mwaka mpya wa fedha 2018/2019 katika mnada wa zao la Ufuta uliofanyika katika viwanja Makao makuu ya wilaya hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti, Alvera Ndabagoye akizungumza kuhusiana na kuongezeka kwa makampuni ya kununua Ufuta katika Wilaya ya Kibiti katika mnada wa zao la Ufuta uliofanyika katika viwanja Makao Makuu ya wilaya hiyo.
 Sehemu ya wakulima na kampuni ziliozoomba ununuzi wa zao la Ufuta.
Viongozi wa Ushirika  wakifungua sanduku la zabuni za maombi ya kampuni za kununua ufuta

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad