HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 23 June 2018

ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE

Na Anthony Ishengoma WAMJW
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa kati ya asilimia 7 na 16 ya wanawake wote duniani ni Wajane.  

Jamii imetakiwa kuendeleza mipango na kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwainua wajane ili wapate uwezo wa kiuchumi wa kuzihudumia familia na wategemezi wao kwa kuwa ndiyo muhimili pekee wa familia iliyoachwa.

Akiongea kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano la Wajane liliofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Bi. Honoratha Rwegasira amepongeza juhudi za wadau wa maendeleo na serikali katika kuwasaidia wajane kuleta usawa wa kinjisia na kuinua ushiriki wao katika ngazi za kutoa maamuzi.  

Aidha Bi.Rwegasira ameitaka jamii kuacha mila potofu kama vile kunyanganya mali mjane, kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo, kurithi wajane na nyingine zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke katika jitihada zake za kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara  ya Afya,Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza amesema kimsingi lengo la maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani ni kutoa nafasi kwa Wadau kushirikiana na Serikali kwa kutoa huduma za msingi kwa wajane na kuondoa aina zote za ukandamizaji ikiwemo haki ya kumiliki mali, umasikini, mira na desturi za kurithiwa baada ya kufiwa.

Aidha Bi. Magwiza ametaja mipango ya baadae ya maadhimisho haya kuwa ni kuhakikisha wajane wanapata haki za msingi,kuainisha maeneo na takwimu za mila na desturi kinzani na haki za wajane mengineyo ni kushawishi wadau kuchangia katika uwezashaji wanawakwe kiuchumi hasa kundi la wajane ili kuondokane na umasikini wa kaya.

Kongamono hilo pamoja na kuwakutanisha Wajane wa Jiji la Dodoma pia limewakutanisha wadau wa masuala ya haki za wajane ambapo Mwakilishi kutoka shirika la TAWIA Bi.Neema Duma ameitaka serikali kuhakikisha wajane wanapewa hati za vifo vya waume zao pia kutaka masuala ya wajane yanashughulikiwa kimkakati zaidi na kuunda mfuko wa wajane wenye umri mkubwa na wale wasiojiweza kabisa.

Tarehe 23, Juni kila mwaka  ni Siku ya Wajane Duniani ambayo chimbuko lake linatokana na mwanaharakati Pushpa Vati Loomba ambaye alishuhudia mama yake akikabiliwa na shida nyingi baada ya kufiwa na mme wake Juni 23, 1954 na kuanzisha Loomba Foundation kwa ajili ya kampeini ya kueleza shida za wajane ambazo hazionekani, zimesahaulika na hazisemwi popote.
 Mkurugezi  Msaidizi  Idara ya Jinsia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza akitoa hutuba yake kwenye  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
 Afisa Mwandamizi  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi .Sirivia Siliwa  akitoa mada kuhusu Chimbuko la  Siku ya  Wajane Duniani wakati wa Kongomano la Wajane lilifanyika leo Mjini Dodoma.
 Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma  Bi. Honoratha Rwegasira  akitoa hutuba ufunguzi  kwa niahaba ya Mgeni rasmi wakati wa  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
Wajane wa Mkoa  wa Dodoma wakiwa kwenye  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad