HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 June 2018

ALIKIBA ATOA TAMBO,ASEMA HAIHOFII TIMU YA SAMATA


Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
ZIKIWA zimesalia siku 2 kuelekea mechi ya hisani kati ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samata, majigambo na mbwembwe zimeshika hatamu.Mechi hiyo ni kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kusaidia kuboresha miundombinu ya mashuleni na kwa kuanzia wataanza na shule walizosoma wao.Alikiba akiwa amesoma shule ya msingi Upanga na Samata akiwa amesoma shule ya msingi Mbagala Rangi Tatu.

Anazungumza leo Jijini Dar es salaam,Alikiba amesema haogopeshwi na timu ya Samata kwani ni ya kawaida na iwapo yeye atataja kikosi chake basi hawataamini masikio yao.

Kiba amesema muda wowote atataja kikosi chake ambapo amesema alitaman baadhi ya wachezaji wa SimbaSC wangekuwepo pia katika kikosi chake ambao kwa sasa wapo nchini Kenya kwa ajili ya mashindano ya Sport pesa.

"Utakuwa ni mchezo wa kiufundi zaidi kwani wachezaji watakaocheza siku hiyo ni wenye viwango" amesema Kiba.Hata hivyo Muwakilishi wa Kampuni ya Asas Fahad Ali amesema kuwa kujumuika pamoja kupitia mpango huo wa mechi hiyo ni kuzidi kutoa mchango wa elimu kwa wanafunzi.

Pia imeelezwa kuwa ili kufanikisha zaidi mchango wanaoukusudia kuupata watanzania wafike kwa wingi siku hiyo kushuhudia burudani hiyo.Mtanange huo utakaochezwa Juni 9 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini na utakaoanza saa 10 jioni kwa kiingilio cha She. 2000 kwa V.I.P na 1000 kwa viti vya kawaida.
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba akizungumza na vyombo vya habari leo katika ukumbi wa viwanja vya taifa Jijini Dar es Salaam kuhusu mchezo utakaochezwa kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi.
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba (katikati) na Uhuru Selemani (kulia) wakiwa wameshikilia jezi waliokabidhiwa na uwongozi wa kampuni ya Asas leo katika ukumbi wa viwanja vya taifa Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad