HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 14, 2018

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA LEO

 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge kuhusu changamoto za Muungano wakati wa kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Picha zote na Daudi Manongi,
 Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt.Florens Turuka  na Naibu Katibu Mkuu Bi.Immaculate Ngwale pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati wa kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Majenerali wastaafu wa Jeshi la Wananchi watanzania(JWTZ)  wakifuatilia kipindi cha maswali  na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Wachezaji wa Timu ya Simba ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu Bara kwa  mwaka 2017/18 wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
 Viongozi wa Timu ya Simba  wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
MAELEZO DODOMA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad