HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 20, 2018

WAKALA WA VIPIMO TANZANIA WAZIKAGUA TOCHI ZA ASKARI USALAMA BARABARANI

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAKALA wa Vipimo Tanzania(WMA) wamefanya ukaguzi wa tochi za Askari wa Usalama Barabarani katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kupima ubora wa vifaa hivyo vya usalama.

Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Vipimo duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo Mei 20 ya kila mwaka ambapo Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa  amesema ukaguzi huo umelenga kupima ubora wa vifaa vya usalama barabarani ili kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani hapa nchini.

Pia amesema kumekuwepo malalamiko kwa watumiaji wa barabara kwa kuamini kuwa tochi zinazotumiwa na askari wa usalama barabarani zinawapunja speed, hivyo wameamua kuzipima ili kuangalia kama ni kweli ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa tochi hizo.

Kwa upande wa Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai amewahimiza madereva kutii sheria bila shuruti ili kupunguza ajali barabarani.

Pia amewatoa hofu watumiaji wa barabarani kuwa tochi zinazotumiwa na askari wa usalama barabarani zimekaguliwa na hazina tatizo, hivyo ni kutii sheria na ukomo wa speed ili kupunguza ajali za barabarani.


Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa tochi za Barabarani  zinazotumiwa Askari wa usalama Barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akionesha mmoja ya tochi wanazotumia askari wa usalama barabarani mara baada ya kufanyiwa ukaguzi na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi  na Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Pwani (ASP),Mossi Ndozero akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tochi zilivyosaidia kupunguza ajali za barabarani ambapo mwaka huu zimepungua sana mkoani humo.
Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) pamoja na Askari wa Usalama barabarani mkoani Pwani wakifanya vipimo vya ubora wa tochi za barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Afisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA)Glory Mtana (katikati) akichukua vipimo vinanyosomwa kwenye tochi za usalama barabarani wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika mkoani Pwani.
Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) Siraji Moyo(kushoto) pamoja na Glory Mtana (kulia) wakihakiki vipimo vinavyotolewa na tochi za barabarani ili kujilizisha wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa(kushoto) akielekezwa  na mmoja wa Polisi wa usalama barabarani mkoani Pwani namna ya kupima spidi ya magari kwa kutumia tochi za Usalama barabarani  wakati wa maadhimisho ya wiki ya vipimo Duniani
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa akipima spidi ya gari kwa kutumia Tochi ya Askari wa Usalama barabarani mara  baada ya kuvifanyia vipimo vifaa hivyo leo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayofanyika Mei 20 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa, Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai, Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) pamoja na askari wa Usalama Barabari wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya ukaguzi wa tochi wanazotumia Askari wa Usalama Barabarani.
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai  akitoa elimu kwa dereva aliyefanya makosa ya barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya vipimo Duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad