HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 25 May 2018

Wahariri na Waandishi wa habari wa mikoa ya Kagera na Geita wafundwa na TFDA

Waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari watakiwa kutumia vyombo vyao kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahii ya vipodozi vyakula pamoja na madawa ili kuweza kuepuka madhara yatokanayo na vitu hivyo.

Hayo yamebainishwa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa nchini.Adam Fimbo wakati wa kikao cha kazi cha wahariri na waandishi wa habari kutoka geita na Kagera kuhusu uhamasishaji wa sheria ya chakula na dawa kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Kagera.

Amesema kuwa kuwepo kwa waandishi wa habari ni moja ya njia ya kuweza kufikisha ujumbe ili kuhakikisha soko la Tnzania linakuwa na bidhaa bora na sanifu na kupitia vyombo vya habari ujumbe utawafikia wananchi juu ya bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA.

Aidha katika hutuba  ya ufunguzi wa kikao hicho mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu amevitaka vyombo vya habari kutoa ushirikiano mkubwa katika kwa kuwa suala la kudhibiti ubora wa dawa na chakula sio jukumu la mamlaka peke yake bali kila mwananchi analo jukumu hilo.

Kijuu amesisitiza kuwa serikali haitasita kumchukulia hatua stahiki yeyote atakayebainika anasambaza na kuuza bidhaa zilizokatazwa na mamlaka kwa kuwa atakuwa anahatarisha maisha ya wananchi waliowengi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Fimbo akiwasilisha hotuba yake kwa wakati wa kikao cha kazi cha wahariri na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Geita na Kagera kuhusu uhamasishaji wa sheria ya chakula na dawa kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu , Salum Kijuu akitoa hotuba yake kwa wajumbe wakati wa kikao cha kazi cha wahariri na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Geita na Kagera kuhusu uhamasishaji wa sheria ya chakula na dawa kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu ,Salum Kijuu akiwa kwenye picha ya pamoja na  wahariri na waandishi wa habari  kutoka Mkoa wa Geita na Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu ,Salum Kijuu akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa  Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA katika  kikao cha kazi cha wahariri na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Geita na Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad