HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 21 May 2018

VIJANA WATAKIWA KUSIMAMA KIIMANI ILI WAFANIKIWE


 Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma akizungumza wakati wa Kongamano la tatu la Panda katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Jijini Dar es Salaam ambapo Taasisi ya Her Initiative iliandaa kongamano hilo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Na Humphrey shao, Globu ya Jamii

Wito umetolewa kwa Vijana kutanguliza ibada kwanza katika shughuli zao za ujasilimali ili waweze kupata mafanikio ya kweli katika maisha .

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu wanaojihusisha na masuala ya ujasiriamali chini ya Taasisi ya Her Initiative.

“ni Vizuri kongamno hili limefanyika katika mwezi huu mtukufu kwani Vijana wengi mnaingia katika biashara na kumsahau Mungu hali inayosababisha kuyumba kimaisha” amesema Vuma.

Ametaja kuwa suala la Imaan lina nafasi kubwa katika maisha ya Vijana kwani itasaidia kupunguza baadhi ya anasa ambazo zinapelekea kula mtaji wako wa baishara.
 
Amesema tatizo tulilonalo vijana wengi wetu hatujui umuhimu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe lakini ni wepesi kuweka bando hata la 30,000 ili mradi usikosekane facebook wala WhatsApp.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux akizungumza na Vijana wa Chuo Kikuu katika Tamasha la Panda TUDARCO.
Muanzilishi wa Kampuni ya Mon Finance, Monica Joseph akieleza umuhimu wa kutunza akiba kwa Vijana ili waweze kufikia mafanikio.
Mtangazaji wa Radio , Meena Ally akiongoza mjadala wakati wa kongamano la Panda.
Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma akikabidhi cheti kwa mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya ujasiliamali.
Sehemu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu waliofika katika kongamano la Panda lililofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad