HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 14 May 2018

Shindano la utunzi wa hadithi la Andika Challenge lazinduliwa

Na Mwandishi wetu
TAASISI ya Dr Ntuyabaliwe imezindua shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni wenye lengo la kuibua vipaji vya watoto katika kubuni na kutunga hadithi.

Shindano hilo linatarajiwa katika siku za usoni kufika Tanzania nzima.

Uzinduzi huo umefanywa katika shule ya msingi Kinondoni wilayani Kinondoni.

Akizindua shindano hilo Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya alisema shindano hilo ni muhimu kwa nchi hii hasa katika kukuza uwezo wa kusoma na kuandika na kuibua vipaji vya wanafunzi katika kukuza lugha ya Kiswahili na ubunifu.

Alisema kwamba serikali inafurahishwa na jinsi taasisi hiyo inavyofanywa ya kuibua vipaji vya watoto na kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia usomaji wa vitabu na shindano la andika challenge.

Alisema anajua kwamba Taasisi hiyo ilianza na maktaba katika shule za msingi na kuhamasisha usomaji wa vitabu na sasa wanakuja na shindano hilo litakalosambaa nchi nzima.

Alisema andika challenge ni muhimu kwa watoto.

“Tunaamini kuwa tunaenda kukuza vipaji vya watoto…katika kutunga hadithi kwa kuongoza watoto katika kuhakikisha kwamba uchaguzi wa mada zinakuwa na maana zikizingatia fani na maudhui, moja ya tanzu au kipera cha simulizi “ alisema.

Alisema hali hiyo iliyoletwa na taasisi hiyo inahamasisha watoto kufikiri na kutaka walezi walimu na wazazi kuona na kuendeleza uibuaji vipaji vya watoto.

Alisema kwa kuwa na mashindano taasisi hiyo inafanya watoto kuwania tuzo na hivyo kuleta hamasa na changamoto katika utunzi na usambazaji wa maudhui.

Alisema kuna faida nyingi na shindano hilo kwa kuwa inakuza lugha kwa kukuza msamiati pia baadhi ya hadithi zitahifadhi utamaduni wetu.

Kuna wazazi watawaelekeza watoto hadithi na hivyo kuhifadhi mila na desturi

Shindano hilo linagusa wanafunzi wa darasa la nne hadi la 7.

Akitoa neno la shukurani mwanafunzi Brian Jackson ambaye anasoma darasa la saba shule ya Kinondoni alimshukuru mama Mengi kwa kuzindua andika challenge .

Alisema anaamini kuwa kwa mashindano hayo ya utunzi wa hadithi  utaibua vipaji na fikira na maarifa na itawapelekea kutundika tunzi mbalimbali za hadithi.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi amesema licha ya Taasisi yake kuhusika na ukarabati wa vyumba vya maktaba na kutoa vitabu kwa shule za msingi, imeamua kuanzisha shindano la ANDIKA CHALLENGE kwa ajili ya wanafunzi wa manispaa za Kinondoni na kabla ya kulipeleka  nchi nzima katika awamu tofauti, ikiwa ni kuunga mkono wa jitihada za serikali za kuboresha elimu nchini.

Amesema shindano hilo kwa wilaya ya Kinondoni litafikia kilele  Mei 30 mwaka huu, na washindi watano wa kwanza watatangazwa na kuzawadiwa tarehe 16 Juni mwaka huu,  wakati wa maadhimisho ya siku ya  mtoto wa Afrika kwa mwaka huu.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga amesema atahakikisha kuwa wanafunzi wengi wa shule yake wanashiriki katika shindano hilo na kutoa wito kwa watoto wengine wilayani humo kuonesha umahiri wao.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akipewa kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga kwa ajili ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga (hayupo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi (kulia) akiongozana na mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya (wa pili kulia), kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga (wa pili kushoto), Mwandishi wa Habari wa IPP Ltd. Abdulhamid Njovu (kushoto) wakielekea kwenye ukumbi wa maktaba ya shule ya msingi Kinondoni kwa ajili ya kuzindua shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga akizungumza machache na kuitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura, Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Elimu kata ya Mwananyamala, Joshua Biswalo wakiwa meza kuu.
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya msingi Kinondoni wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na  Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura (kushoto).
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akitoa mkono wa pongezi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza kuhusu vigezo vya kushiriki na zawadi kwa tano bora kwa wanafunzi wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni watakaoshiriki shindano la Andika Challengekatika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba ya shule ya msingi Kinondoni mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi Brian Jackson wa darasa la saba shule ya msingi Kinondoni akitoa neno loa shukrani kwa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe kwa kuzindua shindano hilo la andika challenge wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanafunzi Blessing Elianoki wa darasa la sita.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo wakati wanafunzi Brian Jackson na Blessing Elianoki walipokua wakitoa neno la shukrani kwa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akiwapongeza wanafunzi  Brian Jackson na Blessing Elianoki waliotoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wanaoshudia tukio hilo Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi (wa tatu kulia), Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga (wa pili kulia), Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura (kulia) pamoja na Afisa Elimu kata ya Mwananyamala, Joshua Biswalo (kushoto).
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakizundua shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akimpongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi mara baada ya kuzindua rasmi shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waandishi wa habari na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni waliohudhuria uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kinondoni waliowakilisha wenzao katika hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliowakilisha wenzao katika hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad