HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 18, 2018

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO MPAKA KATI YA MANYARA NA TANGA

Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Serikali yamaliza mgogoro wa mpaka kati ya mkoa wa Manyara na Tanga katika wilaya za Kiteto na Kilindi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi ambaye amesema moja ya sababu kubwa za kuwepo kwa mgogoro huo ni baadhi ya wapimaji mipaka waliokuwepo wakati huo kuhongwa na kupindisha mpaka.

Mgogoro huu uliwasilishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati alipofanya ziara yake mwezi januari mwaka 2017 ambapo wananchi walifikisha malalamiko ya mgogoro huo ambao umegharimu maisha ya watu wengi na mauaji ya mara kwa mara.

Waziri Mkuu alimtaka wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushirikiana na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuunda timu ya wataalamu ambao walianza kazi ya upimaji mwezi Machi 2017 ambao walipima mpaka huo kwa usahihi japo na wao walitaka kuhongwa pesa kutoka kwa baadhi ya watu hata hivyo walizikataa.

Akiwatangazia wananchi waliohudhuria katika mkutano huo Waziri Lukuvi aliwatangazia wananchi kwamba Mgogoro huo kwa sasa umeisha na kwa sasa serikali itaweka mipaka mipya inayozingatia maslahi ya pande zote mbili.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo amewataka wananchi wote wa wilaya zote mbili kuishi kwa amani na kuondoa tofauti zao za hapo awali kwa kuwa mgogoro huo umesababisha maafa mengi na asingependa kuona yanajirudia kwani wote ni watanzania.

Wakazi wa wilaya hizo mbili wamemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo kwa kusimamia hatma ya mgogoro huo na wameahidi kuishi kwa amani.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiongea na wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wakati akiwatangazia kuhusu Serikali kumaliza mgogoro wa mpaka wa wilaya hizo mbili.
   Eneo la mpaka wa Kiteto na Kilindi ambalo lilikuwa na mgogoro
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akisalimiana na wakazi wa wilaya za Kiteto na Kilindi wenyenyuso za furaha mara baada ya kumalizika kwa mgogoro huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo akisalimiana na wakazi wa wilaya za Kiteto na Kilindi wenyenyuso za furaha mara baada ya kumalizika kwa mgogoro huo.
  Baadhi ya wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wa utatuzi wa mgogoro kati ya wilaya hizo wakifuatilia kwa makini maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huo.
 wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wa utatuzi wa mgogoro kati ya wilaya hizo wakifuatilia kwa makini maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huo.
 Baadhi ya wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wa utatuzi wa mgogoro kati ya wilaya hizo wakifuatilia kwa makini maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo wakiteta na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela. Picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad