HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 8 May 2018

NG'UMBI AVISHWA RASMI CHEO CHA BRIGEDIA JENERALI

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa  Kairuki kwa niaba ya Makao Makuu ya Jeshi amemvisha  rasmi Kanali R.C Ng’umbi  cheo kipya cha  Brigedia Jenerali.

Brigedia Jenerali Ng’umbi  ambaye pia ni Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Tanzania  nchini China , ni miongoni mwa maofisa  27 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo  tarehe 12 Aprili mwaka ,2018 na Rais na Amiri Jeshi  Mkuu Dkt. John Magufuli.

 Akizungumza Mara baada ya kuvalishwa Cheo hicho jana Mei 7 , Brigedia Jenerali  alimshukuru Amiri Jeshi Mkuu  Dk. Magufuli  pamoja na uongozi wa Makao Makuu ya Jeshi kwa kupandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.

Tukio hilo lilifanyika  katika ofisi za  ubalozi wa Tanzania nchini China  na kuhudhuriwa na maofisa  pamoja na watumishi  kutoka ofisi  za Ubalozi  pamoja na familia zao.
 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa  Kairuki kwa niaba ya Makao Makuu ya Jeshi akimvisha  rasmi Kanali R.C Ng’umbi  cheo kipya cha  Brigedia Jenerali katika hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini China.
  Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa  Kairuki, Brigedia Jenerali, R.C Ngumbi  wakiwa katika picha ya pamoja  na Maafisa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.
  Brigedia Jenerali R.C Ngumbi akiwa katika  picha ya pamoja  na Balozi Mbelwa Kairuki, Maafisa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad